Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo (20.09.2012) | Makala | DW | 20.09.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Makala

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo (20.09.2012)

Wahariri leo wamejishughulisha na mada kuhusu kuchapishwa kwa vibonzo vya mtume Mohammad na jarida la Charlie Hebdo la Ufaransa. Wahariri pia wanazungumzia kutolewa kwa data mpya za manazi mambo leo hapa Ujerumani.

Kuhusu kuchapishwa kwa katuni za Mtume Muhammad, gazeti la Frankfurter Allgemeine linasema hatua hiyo imeibua hofu juu ya uwezekano wa kutokea machafuko mapya. Mhariri wa gazeti hilo anasema kumezuka mjadala mpya wenye utata ikiwa kila wachoraji wa katuni wa aina hiyo wanaosababisha uchochezi na wanaofanya hivyo kwa kudai wana uhuru wa kufanya hivyo, kama pia wana uhuru wa kutofanya jambo lolote linaloweza kuwa na athari. La busara lingekuwa kutulia katika hali hii ya wasiwasi iliyojitokeza badala ya kutaka uhuru wa kujieleza ubanwe kidogo kuepusha ghadhabu miongoni mwa watu wanaokwazwa nafsi zao.

Nalo gazeti la Ludwigsburger Kreszeitung linasema pendekezo la kuimarisha sheria kuhusu unafiki wa kidini kwa wakati huu kungekuwa ni kutoa haki isiyostahiki. Mhariri wa gazeti hilo anatilia maanani kwamba mjadala wa aina hiyo unaweza kufanyika wakati hali itakapotulia na kuzungumzia mipaka ya kuvumiliana miongoni mwa watu wote katika jamii. Wakristo, Waislamu, Wayahudi na hata wale wasiokuwa wafuasi wa dini yoyote. Na bila shaka pia kuhusu mipaka ya stahamala na uvumilivu nchini Ujerumani.

Gazeti la Rheinische Post la mjini Düsseldorf linasema demokrasia kama Ufaransa lazima ilinde uhuru wa maoni na wa vyombo vya habari. Gazeti linasema kujificha kwa hofu ya kutokea machafuko na kutochukua hatua yoyote, ni kutoa mwanya kwa shinikizo la itikadi kali za kidini. Hilo linaweza kutokea lakini halipaswi kuruhusiwa. Uhuru wa vyombo vya habari unajua mipaka yake, hususan kama unakandamizwa au kudhalilishwa. Lakini katuni za Mtume Mohammad zimechapishwa katika mazingira tofauti: wakati maandamano yakiendelea katika mataifa ya kairabu kufuatia filamu inayoudhalilisha Uislamu. Ni kama kuongeza mafuta kwenye moto. Mhariri anamalizia kwa kusema kuna mazingira fulani ambapo jambo la busara na la rahisi kabisa ni kufunga bakuli lako.

Data kuhusu manazi mambo leo

Mada ya pili iliyowazingatiwa na wahariri leo ni kutolewa kwa data mpya kuhusu manazi mambo leo. Gazeti la Rhein-Necker linauliza je kutolewa kwa data hizo ni hatua kubwa katika vita dhidi ya watu wenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia Ujerumani? Mhariri anasema kuchapishwa data mpya za manazi mambo leo ni juhudi ya kutilia shaka, inayofunika matatizo halisi ya kimsingi yanayozikabili idara za usalama za Ujerumani. Hatua ya muhimu ni kufanya mageuzi yanayohitajika. Na mwito huu unaweza kurudiwa kila mara.

Nalo gazeti la Badische linauliza, je data za manazi mambo leo zingeweza kuzuia ugaidi wa kundi la National Social Underground, NSU? Pengine lakini kwa kiwango kidogo sana, kwa sababu kwa miaka kadhaa idara za usalama zilionya na si mara moja, kwamba kundi la manazi mambo leo linahusika na mauaji ya wahamiaji tisa.

Lakini mhariri anasema kinyume kabisa maafisa wa usalama wakawa wakilitafuta kundi la mafia la Kituruki. Pengine data hizo zimesaidia kuwasaka wanachama watatu wa kundi la manazi mambo leo kutoka Jena - Mundlos, Böhnhardt na Zschäpe. Haikujulikana kwa kiwango gani watu hawa walikuwa hatari, lakini hata hivyo walitafutwa. Mhariri anasisitiza kuwa data zinaweza kuwa na umuhimu kwa maafisa wa usalama katika kuweka wazi zaidi miundo, mitandao na mafungamano ya manazi mambo leo.

Mwandishi: Josephat Charo/Inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman