Maoni: Baada ya ″mapinduzi″ Ethiopia, anakuja mfalme Abiy? | Matukio ya Afrika | DW | 24.06.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Maoni: Baada ya "mapinduzi" Ethiopia, anakuja mfalme Abiy?

Baada ya mgogoro wa mwishoni mwa wiki nchini Ethiopia, waziri mkuu Abiy Ahmed na serikali yake wanaweza kuibuka imara zaidi, anasema mkuu wa idhaa ya Amhariki ya DW Ludger Schadomsky.

"Upeo mpya wa matumaini", ndiyo maneno yaliopo kwenye makaratasi ya barua ya serikali ya Ethiopia iliyoundwa mwaka mmoja uliyopita. Lakini swali ni je, baada ya mgogoro wa umuagji damu mwishoni mwa wiki, matumaini hayo ya Ethiopia ya kidemokrasia iliyoungana yametoweka?

Ni mapema mno kuharakisha kutangaza mwisho wa mabadiliko baada ya kinachoelezwa kuwa mapinduzi au jaribio la mapinduzi. Lakini mauaji ya kikomandoo dhidi ya maafisa watano wa juu wa serikali yanazusha maswali mazito kuhusu uwezo wa kidemokrasia wa taifa hilo la pembe ya Afrika lenye wakaazi zaidi ya milioni 100.

Mradi wa uchaguzi umeshindwa kwa sasa

Mambo mengi yalionekana kuwa na uhakika.  Uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika Mei 2020 hautafanyika tena kama ilivyopangwa, na hata zoezi la sensa lililaazimika kufutwa hivi karibuni. Shauku ya Abiy juu ya kuidhinishwa kwa mageuzi yake na wapigakura kwa hiyo imeshindwa.

MA-Bild Ludger Schadomsky (DW/P. Böll)

Mkuu wa idhaa ya Amhariki ya DW, Ludger Schadomsky.

Kiongozi huyo mpya anaonekana dhaifu pia kwingineko: Machafuko ya kikabila yanafukuta nchini kote, na Ethiopia yenye mamilioni ya watu waliokosa makaazi, ni mahala pa idadi kubwa ya wakimbizi barani Afrika. Inawezekana bado kuunda taifa kwa kiongozi dhaifu kama huyo?

Lakini kuna tafsiri mbadala ya namna matukio ya karibuni yatakavyounda historia ya Ethiopia - baada ya hisia za ubora wa kikabila zilizokandamizwa kwa karne kadhaa kuibuka tena.

Waziri Mkuu Abiy, ambaye alianza kama msuluhishi, hivi sasa ndiye anadhibiti mambo. Nafasi za wakuu wa majimbo, jeshi na usalama wa taifa zote zinadhibitiwa na watu wa karibu wa Abiy. Badala ya kuonekana kama mtu asiejua chochote, mwanamageuzi huyo kijana ametenegeza ramani ambayo wananchi wameitaka kwa muda mrefu.

"Mfalme Abiy"

Mwishowe, waumini wa nadharia hii wanatabiri, kiongozi huyo wa serikali atageuka kuwa mfalme mwenye mamlaka yote. Na si tayari amekwishaonyesha mapenzi na madaraka ya urais?

Mfalme Abiy njiani? Bado haujafika muda huo, na hatuwezi kuzungumzia katika mazingira yoyote yale, kurejea kwenye utawala wa zamani wa mkono wa chuma. Lakini ikiwa mradi mpya wa matumaini utafanikiwa, itahitajika maandishi ya wazi zaidi kutoka juu. Na utayarifu wa wa Ethiopia milioni 105 kuunga mkono mradi huo wa kihistoria mbali ya mipaka ya kikabila.