Mandela atimiza miaka 92. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 18.07.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Mandela atimiza miaka 92.

Julai 18, siku aliyozaliwa Nelson Mandela, ambayo sasa ni siku ya Kimataifa duniani.

default

Nelson Mandela atimiza miaka 92.

Leo, Nelson Mandela, Rais wa Kwanza mwenye asili ya Kiafrika nchini Afrika Kusini ametimiza miaka 92 ya kuzaliwa, huku ulimwengu ukisherehekea siku ya kwanza ya kimataifa iliotengwa kwa heshima ya Mandela. Viongozi wa dunia na watu wa kawaida nchini Afrika Kusini na kote ulimwenguni, wamejitolea kutenga dakika 67, leo kutoa huduma kwa umma, kukumbuka miaka aliyotumia Mandela katika harakati za kisiasa. Mwaka uliopita Umoja wa Mataifa uliitambuwa siku ya leo ya kuzaliwa kwa Mandela  tarehe 18 Julai kuwa siku ya kimataifa ya Nelson Mandela, na itasherehekewa kote ulimwenguni. Baada ya kuachiliwa huru mwaka wa 1990, Mandela ambaye aliongoza vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini alichaguliwa kama rais wa kwanza wa kiafrika nchini humo hapo mwaka 1994. Leo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa na jamaa zake, nyumbani kwake mjini Johannesburg.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com