Mamia waachwa bila makao kufuatia machafuko mapya Haiti
12 Mei 2026
Watu hao wanadaiwa kukita kambi katika barabara inayoelekea uwanja mkuu wa ndege wa nchi hiyo.
Hospitali katika mji wa Cite Soleil ziliwahamisha wagonjwa wake na shirika la misaada la Madaktari Wasio na Mipaka la MSF limesimamisha kutoa huduma zake katika eneo hilo. Machafuko hayo ya magenge yaliibuka mwishoni mwa wiki katika mitaa kadhaa ya mji mkuu.
Polisi inasema kuwa magenge hayo yametanua operesheni zake ikiwemo uporaji, utekaji nyara, udhalilishaji kingono na ubakaji hadi katika maeneo ya vijijini.
Haiti haijawa na rais tangu kuuwawa kwa Rais Jovenal Moise mnamo Julai 2021.
Ripoti iliyochapishwa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM mapema mwaka huu ilisema kuwa machafuko ya magenge yamewapelekea watu milioni 1.4 kuyakimbia makaazi yao nchini Haiti.