Abla Pokou ni malkia aliyeuongoza msafara wa watu wake kutoka eneo ambalo leo hii ni Ghana hadi Ivory Coast. Alipofika huko aliazisha taifa la watu wa Baoule mnamo mwaka 1770. Simulizi zinadai kuwa alimrusha mtoto wake pekee kwenye maji ya Mto Comoé ili watu wake waweze kuuvuka.