MAKKAH: Mahujaji wafika kwenye Mlima Arafat | Habari za Ulimwengu | DW | 29.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MAKKAH: Mahujaji wafika kwenye Mlima Arafat

Nchini Saudi Arabia mahujaji takriban milioni tatu wamewasili kwenye Mlima wa Arafat, nje ya mji mtakatifu wa Makkah, kushiriki kwenye ibada ya kutwa nzima mwanzoni mwa Hija ya mwaka huu.

Mtume Mohammed SAW alitoa khutba yake ya mwisho katika mlima huo, kiasi miaka alfu moja na mia nne iliyopita.

Ibada ya leo ambapo mahujaji wanaomba msamaha kwa Mola wao ndio upeo wa Hija iliyoanza jana na itakayokamilika siku ya jumatatu.

Taratibu mpya za usalama zimeandaliwa mwaka huu kwa nia ya kuzuia misongamano ambayo imewahi kusababisha maafa makubwa katika Hija za miaka iliyopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com