1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makamu wa rais wa zamani wa Equador ahamishiwa gereza

11 Novemba 2025

Equador imewahamishia wafungwa 300 walio kwenye hatarini kwenye gereza jipya lenye ulinzi mkali zaidi, akiwemo makamu wa zamani wa rais, Jorge Glas, siku moja baada ya wafungwa 31 kuuawa.

https://p.dw.com/p/53PK4
Jorge Glas
Makamu wa zamani wa rais wa Equador, Jorge Glas, amehamishiwa gereza baada ya wafungwa zaidi ya 30 kuuawa.Picha: JUAN RUIZ/AFP

Uhamishaji huo ni sehemu ya mpango wa Rais Daniel Noboa kuyadhoofisha magenge ya kihalifu amabyo yamekuwa yakiendesha shughuli zao ndani ya magereza ya nchi hiyo ya Amerika Kusini kwa muda mrefu.

Mamia ya wafungwa wamepoteza maisha kutokana na magenge hayo katika miaka ya hivi karibuni.

Rais Noboa alichapisha  picha ya Glas akiwa kwenye gereza hilo jipya katika mtandao wa X, hatua iliyolalamikiwa na wakili wa makamu huyo wa zamani wa rais kama kitendo cha uvunjaji haki za binaadamu.

Mnamo mwezi Juni, mahakama ilimuhukumu Glas kifungo chengine cha miaka 13 kwa ubadhirifu wa fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa maeneo yaliyoathirika kwa tetemeko la ardhi.