You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Iran
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Picha: Zoonar/picture alliance
Makala zetu
Sikiliza makala kemkem tulizokuandalia
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Afrika wiki hii
Baraza kuu la UN lapitisha azimio la kutambuwa utumwa kama uhalifu mbaya zaidi uliofanywa dhidi ya waafrika. Tanzania, aliyekuwa waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera bunge na wenye ulemavu William Lukuvi amefariki dunia. Na Kenya yagunduwa kaburi la pamoja lililozikwa miili ya watu 33. Jiunge na Saumu Mwasimba katika makala ya Afrika wiki hii
Vijana Tugutuke: Vijana Assembly kutoa elimu ya kutunza maji
Kundi la Vijana Assembly wanavyotoa elimu ya kutunza maji kwa jamii ya Masai huko Monduli mkoani Arusha nchini Tanzania.
Mtu mmoja auwawa katika maandamano ya nchini Kenya
Kenya yatikiswa na maandamano makubwa katika mji mkuu Nairobi na miji mingine ya kupinga muswaada wa fedha. Mahujaji 658 wa Misri ni miongoni mwa waumini waliopoteza maisha kufuatia joto kali huko Makkah. Wabunge nchini Kongo wakubali kupunguziwa mishahara yao ya dola elfu 21 hadi dola elfu 5 katika tukio la aina yake. Jiunge na Saumu Mwasimba katika Afrika wiki hii hapa DW kiswahili.
Makala ya Afrika Wiki HII
Afrika Wiki hii ina mengi ikiwemo athari ya vikwazo vya Marekani kwa jeshi la Rwanda. Mtayarishaji ni Amina Abubakar
Mwangaza wa Ulaya: Mfumo wa kutoa tahadhari mtoto akipotea
Mfumo wa kipekee uliobuniwa miaka 20 iliyopita nchini Ufaransa ambao pia unatumiwa katika mataifa mengine ya Ulaya unaohusu kutoa tahadhari ya kitaifa pale kunaporipotiwa utekaji nyara wa watoto au hata taarifa ya mtoto kupotea. Miaka 20 tangu kuanzishwa kwake, mfumo huu unaofahamika kwa kiingereza kama "Child abduction alert" umeendelea kutoa matokeo chanya katika suala zima la kuwalinda watoto.
Makala ya Afrika wiki hii
Suala la vijana wa Kiafrika kurubuniwa na kusafirishwa hadi Urusi ili kupigana vita nchini Ukraine. Tanzania ilisema kuwa vurugu zilizoshuhudiwa nchini humo wakati wa uchaguzi ni miongoni mwa mada zilizojadiliwa katika mkutano wa marais wa Umoja wa Afrika. Na makabiliano yaendelea kuripotiwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo licha ya miito ya usitishwaji mapigano.
Makala ya Afrika wiki hii
Kipindi kinachoangazia matukio ya wiki yaliyoripotiwa kuhusu na kutoka barani Afrika.
Afrika Wiki Hii
Miongoni mwa yaliyotikisa Afrika ni pamoja na kauli ya Rais Paul Kagame ya kutaka Wanyaranwa kujitegemea zaidi.
Makala ya Afrika Wiki Hii
Makala ya Afrika Wiki Hii ikiyaangazia matukio yaliyoripotiwa kuhusu na kutoka Afrika.
Mwangaza wa Ulaya: EU na Marekani zavutana kuhusu Greenland
Kipindi hiki cha Mwangaza wa Ulaya kinaangazia namna mvutano kati ya nchi za Ulaya na Marekani kuhusu Greenland ulivyosababisha mabadiliko ya sera na azma mpya ya nchi za Ulaya kujitegemea zaidi kiusalama na kutaka kurejesha uhusiano na jirani yao Urusi. Hii itakuwa na athari gani?
Makanisa yanavyofungwa Ujerumani kwa kukosa waumini
Makanisa mengi ya Ujerumani yanaendelea kufungwa kwa kasi tofauti na miaka ya nyuma. Sababu kubwa za kufungwa kwa nyumba hizo za ibada ni zinatokana na uhaba wa waumini na gharama kubwa zilizoshindikana za kuzitunza. Ungana na Angela Mdungu katika makala ya Sura ya Ujerumani kufahamu zaidi.
Makala: Afrika Wiki Hii
Afrika Wiki hii: Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo katika baraza lake la mawaziri +++Huko Goma yamefanyika maziko ya miili ya watu 22 waliofariki katika mashambulizi ya droni+++Amnesty International lavishutumu vyombo vya usalama vya Uganda kwa kuendeleza ukandamizaji dhidi ya upinzani.
Fahamu zaidi kuhusu roboti CLOiD linaloweza kukunja nguo
Roboti CLOiD lina uwezo wa kufanya kazi kadhaa za nyumbani ikiwemo ya kukunja nguo. Utasikia pia kuhusu roboti Oto linaloweza kukupokea na kuchangamsha mara tu unapowasili hotelini. Ungana na Angela Mdungu katika makala ya Sema Uvume kufahamu zaidi.
Mwangaza wa Ulaya: Marekani yatishia kuinyakua Greenland
Kumezuka hali ya wasiwasi na ukosoaji kote barani Ulaya kufuatia vitisho vya rais Donald Trump kwamba Marekani itachukua udhibiti wa eneo la Greenland lenye utajiri wa madini na lililopo chini ya himaya ya Denmark.
Makala: Afrika Wiki Hii
Miongoni mwa yaliyomo kwenye Afrika Wiki hii, hali ya siasa nchini Tanzania+++Viongozi wa Kongo na Rwanda watia saini makubaliano ya amani nchini Marekani +++ Utawala wa kijeshi Guinea Bissau watetea hatua yake ya kuchukua madaraka+++ Na hali ya kisiasa Uganda kuelekea uchaguzi Mkuu.
Makala: Afrika Wiki Hii
Sikiliza makala ya Afrika Wiki Hii. Amina Abubakar anadurusu matukio muhimu yaliyotokea Afrika ndani ya juma moja.
Ujasiriamali wa kidijitali unavyochangia uchumi Tanzania
Namna kampuni za ujasiriamali wa kidijitali zinavyofanya juhudi kuchangia maendeleo na uchumi nchini Tanzania.
Makala ya Afrika wiki hii
Nchini Tanzania sakata la kupotea kwa aliyekuwa Balozi wa nchi hiyo nchini Cuba Humprey Polepole laendelea kugonga vichwa vya habari. Utasikia yanayoendelea katika mzozo wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na maandamano ya vijana wenye hasira huko Morocco na Madagascar.
Maoni: Makubaliano ya kusimamisha vita vya miaka miwili Gaza
Wapalestina na familia za mateka wa Israel wamefurahia mapatano yatakayowezesha kubadilishana mateka na wafungwa.
Zifahamu sheria za Ujerumani zinazoweza kukushangaza
Ujerumani ina ruksa ya kufanya mambo mengi yasiyoruhusiwa nchi nyingine. Mtu anaweza kuota jua akiwa utupu kwenye baadhi ya maeneo maalumu, na vijana wenye miaka 16 wanaruhusiwa kisheria kunywa pombe tofauti na nchi nyingine. Hata hivyo ziko sheria zinazoweza kukushangaza. Sikiliza kufahamu zaidi.
Jukwaa la Manufaa
DW Kiswahili inakupa wasaa mzuri wa kuyapeperusha hewani maoni yako yakiwa ni pamoja na kero, ushauri au pongezi kuhusu masuala kadha wa kadha yanayoizunguka jamii yako. Ungana na Angela Mdungu anayekupandisha jukwaani leo.
Makala ya Afrika wiki hii
Mahakama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imemhukumu kifo aliyekuwa Rais wa taifa hilo Joseph Kabila+++Huko Tanzania, joto la uchaguzi mkuu linazidi kupanda+++Maandamano yanayoongozwa na vijana yazitikisa Madagascar na Morocco.
EU yasisitiza umuhimu wa ulinzi dhidi ya droni
Umoja wa Ulaya umesisitiza umuhimu wa kuwekeza katika ulinzi dhidi ya ndege zisizo na rubani barani Ulaya. Lakini Jumuiya hiyo imesema itachukua muda mrefu zaidi ili kujenga uwezo wa ulinzi madhubuti dhidi ya mashambulizi ya droni.
Je Love Bite inaweza kusababisha kiharusi?
Love Bite, au alama nyekundu inayotokana na busu kali kwenye ngozi huzingatiwa kama ishara ya mapenzi. Inapowekwa shingoni na alama kubakia mwilini hugandisha damu kwenye mshipa wa carotid na kusababisha kuziba kwa mtiririko wa damu kwenda kwenye ubongo.
Miwani ya kidijitali inayotafsiri na kupiga picha
Miongoni mwa vifaa vya kisasa zaidi vya kidijitali ambavyo vimeingia kwenye ulimwengu wa bidhaa zinazotumia Akili mnemba hivi sasa ni miwani ya kidijitali ya Rokid inayoweza pia kutafsiri lugha. Ungana naye Angela Mdungu kufahamu zaidi katika makala ya Sema Uvume.
Teknolojia ya usalama ya kulinda mifugo dhidi ya wizi
Kufuatia eneo la Kaskazini mwa Kenya kukumbwa na matukio ya mara kwa mara ya wizi wa mifugo, wanafunzi wa eneo hilo wamebuni mfumo wa kiusalama wa kusaidia kulinda mifugo yao dhidi ya wizi. Hii inatoa taswira ya namna kizazi kipya cha jamii ya wafugaji kinavyochangia ubunifu wa teknolojia katika jamii zao.
Wanawake wajasiriamali wa baharini Zanzibar
Utafiti wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) Tanzania ulibaini kuwa wanawake huchangia zaidi ya asilimia 78 ya kazi za usindikaji wa samaki, uvuvi mdogomdogo, kutembeza watalii na kilimo cha mwani. Makala ya Wanawake na Maendeleo inawaangazia wanawake wanaojishughulisha na ujasiriamali wa baharini.
Athari ya upungufu wa wauguzi Kenya
Watafiti nchini Kenya wanatahadharisha kuwa upunguvu wa wauguzi unachangia vifo vya watoto wachanga kutokana na migomo ya wauguzi hao inayofanyika mara kwa mara, wakidai nyongeza ya mishahara na mazingira mazuri ya kufanyia kazi.
Makala ya Afrika wiki hii
Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Dar es Salaam yatupilia mbali mapingamizi ya mwenyekiti wa chama cha upinzani CHADEMA Tundu Lissu kuhusu kesi ya uhaini inayomkabili +++ Rwanda yasema makubaliano ya Doha na Washington yanayolenga kuutatua mzozo wa mshariki mwa Kongo huenda yasifanikiwe+++Raia wa Malawi wamepiga kura katika uchaguzi uliotawaliwa na ushindani mkali.
Mfahamu Waziri wa Albania aliyetengenezwa kwa Akili Mnemba
Makala ya Sema Uvume, mara hii inamuangazia Waziri wa aina yake aliyetengenezwa kwa kutumia teknolojia Akili Mnemba nchini Albania. Waziri huyo Diella, mwenye muonekano wa mwanamke aliyevalia mavazi ya kiutamaduni ana jukumu kubwa la kusaidia kuidhibiti rushwa hasa katika kutoa zabuni za serikali. Ungana na Angela Mdungu kufahamu zaidi.
Mwangaza wa Ulaya: Luteka ya kijeshi ya Urusi na Belarus
Kipindi cha Mwangaza wa Ulaya kinaangazia luteka ya kijeshi ya pamoja ya Urusi na Belarus iliyopewa jina "Zapad 2025" na athari zake. Ungana na Bakari Ubena.
Makala ya Afrika wiki hii
Ethiopia yazinduwa bwawa kubwa la mradi wa kuzalisha umeme Afrika. Mahakama Kuu Masijala ya Dodoma yamrejesha kwenye kinyang'anyiro cha urais mgombea wa chama cha ACT-Wazalendo Luhaga Mpina. Na mvutano mpya wa kisiasa wanukia Sudan Kusini baada ya serikali kumshtaki makamu wa kwanza wa rais Riek Machar na kumvua majukumu ya uongozi. Sikiliza makala ya Afrika wiki hii na Saumu Mwasimba.
Uchawi na ushirikina katika siasa barani Afrika
Uchawi na ushirikina ni hali inayoendelea kuathiri siasa barani Afrika. Baadhi ya wanasiasa hutuhumiwa kutumia waganga wa kienyeji kutafuta nguvu za kisiasa. Wanasiasa hao huamini kwamba uchawi unaweza kuwasaidia kushinda uchaguzi au kuzuia wapinzani huku wengine wakiamini kuwa uchawi unaweza kuzuia mikosi kutoka kwa wapinzani. Lubega Emmanuel anaangazia hali hiyo katika Makala Yetu Leo.
Hofu ya kujifungua yawakumba wanawake Tanzania
Hofu ya kujifungua ni hali inayowakumba wanawake wengi hasa wale wanaojifungua kwa mara ya kwanza. Wanawake hupata mchanganyiko wa wasiwasi wa kimwili, kihisia na kiakili unaotokana na matarajio ya maumivu, hatari za kiafya au hadithi za kutisha kutoka kwa wanawake wengine waliowahi kujifungua. Veronica Natalis anaangazia kadhia hiyo katika Makala ya Afya Yako.
Athari za madawa ya kuua wadudu kwa nyuki
Madawa ya kuua wadudu hasa yale yanayotumika kwenye kilimo yanaendelea kuwa tishio kubwa kwa uzalishaji wa asali nchini Rwanda. Ingawa lengo la madawa hayo ni kulinda mazao dhidi ya wadudu waharibifu, athari zake kwa nyuki ni hasi na zinaweza kudhoofisha sekta nzima ya ufugaji wa nyuki. Sylivanus Karemera anasimulia katika Makala ya Mtu na Mazingira.
Vijana na teknolojia ya Akili Mnemba Nigeria
Vijana nchini Nigeria wanajituma kufanya ubunifu katika teknolojia hasa ya akili mnemba ili kupata ufumbuzi wa masuala mbalimbali kwenye jamii yakiwemo ya elimu, nishati, usalama, kilimo na huduma za afya. Makala ya Sema Uvume inaangazia hayo.
Sekta ya magari Ujerumani inavyopambana kurudi kileleni
Watengenezaji wa magari Ujerumani wamekuwa wakijikongoja kwa zaidi ya muongo mmoja. Mwanzoni mwa mwaka 2025 takwimu zilionesha kampuni kubwa ya magari ya Ujerumani Volkswagen, inauza magari mengi ya umeme. Sura ya Ujerumani inahoji ikiwa sasa sekta hiyo muhimu inaelekea kupona au la.
Jukwaa la Manufaa
Ni wakati mwingine mzuri kwa wadau wa Jukwaa la manufaa kutoa na kuyasikia maoni yao yanayojumuisha kero dukuduku, ushauri bila kusahau pongezi kuhusu yale yote yanayojiri kwenye jamii. Nahodha jukwaani kwa wakati huu ni Angela Mdungu, ungana naye kusikiliza.
Njia za kukabiliana na hofu ya kujifungua kwa mara ya kwanza
Kwa wanaojifungua kwa mara ya kwanza wakati mwengine wanakuwa na hofu kubwa ya kupitia mchakato mzima wa kujifungua. Wengi wanakuwa na uwoga baaada ya kuwasikia wanawake wengine wakizungumzia mchakato huo wa uzazi. Makala ya Afya Yako inakueleza njia za kukabiliana na hofu hiyo.
Ngoma za Njuga na jinsi zinavyorithishwa kupitia sanaa
Ngoma za Njuga ni aina ya ngoma za asili zinazochezwa kwa kuvaa njuga miguuni au mikononi, zikitamba kwa sauti ya kipekee inayochochea furaha, heshima na mdundo wa kuvutia. Alex mchovu anakupa umuhimu wa ngoma hizo na jinsi ya kuendeleza na kurithisha mila na tamaduni kupitia vipengele vya sanaa.
Makala ya Afrika Wiki Hii
Joto la kisiasa Tanzania linaendelea kupanda kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29. Rais anaetetea kiti chake, Samia Suluhu Hassan, haonekani kuwa na mtihani mkubwa sana kwa kuwa vyama vikuu viwili vya upinzani hadi sasa havina wagombea. Katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo Jeshi bado linapambana na makundi ya wanamgambo na Morocco ndio mabingwa wa mashindano ya Kombe la CHAN-2024
Mkwamo wa soka la Wanawake visiwani Zanzibar
Soka la wanawake Zanzibar linakumbwa na changamoto kadhaa zinazozuia ukuaji wake licha ya vipaji vilivyopo visiwani humo. Hali ya uwekezaji duni imeathiri pakubwa ustawi wa wachezaji, uwepo wa viwanja vichache na ukosefu wa udhamini wa kutosha kwa timu za wanawake. Najjat Omar anaangazia hali ya soka la wanawake Zanzibar.
Mwelekeo wa magari ya umeme EVs nchini Kenya
Magari ya umeme nchini Kenya yanaanza kuchukua nafasi kubwa katika sekta ya usafiri huku juhudi za serikali na kampuni binafsi zikichochea mabadiliko kuelekea nishati jadidifu. Hata hivyo kuna wasiwasi miongoni mwa madereva kuhusu upatikanaji wa miundombinu ya kuchaji, hasa nje ya miji mikuu. Makala ya Sema Uvume yanaangazia hamasa ya kuendana na mabadiliko ya kidijitali nchini Kenya.
Zanzibar - Kisiwa maarufu cha viungo duniani
Zanzibar inasifika kwa uwepo wa mashamba ya viungo ambapo wageni hujifunza kuhusu karafuu, mdalasini, vanila na viungo vyingine vinavyokifanya kisiwa hicho kuwa kitovu cha biashara ya viungo kimataifa. Viungo hivyo hutumika katika tiba, mapishi na ni mojawapo ya utamaduni wa jadi visiwani Zanzibar. Makala ya Utamaduni na Sanaa inamulika jumba la makumbusho la viungo visiwani humo.
Utamaduni wa jamii ya Wasuba nchini Kenya
Jamii ya Wasuba nchini Kenya ni mojawapo ya makabila ya asili yaliyo na historia ya kipekee na tamaduni tajiri, ingawa kwa sasa jamii hiyo inakabiliwa na changamoto ya kutambuliwa na kuhifadhi utambulisho wao wa kitamaduni. Kwenye Makala ya Utamaduni na Sanaa, Musa Naviye anaiangazia jamii ya Wasuba wanaojitambulisha pia kama Abasuba.
Jukwaa la manufaa
Yasikie maoni uliyotutumia msikilizaji yakijumuisha kero, ushauri na hata pongezi kuhusu masuala kadha wa kadha yanayoendelea kwenye jamii yako kupitia Jukwaa la Manufaa. Ungana naye Angela Mdungu kwa takriban dakika tisa za kipindi hiki akiyapeperusha hewani maoni yako.
Afrika wiki hii
Nchini Tanzania kesi dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu imepelekwa Mahakama kuu+++Wabunge nchini Kenya waghadhabishwa na madai ya Rais William Ruto kwamba baadhi yao huchukua hongo ili kupitisha miswada bungeni+++ Amnesty International yashutumu makundi ya waasi na makundi yanaoshirikiana na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa ukatili dhidi ya wanawake na mauaji holela ya raia.
Programu inayotumia Akili Mnemba kutafsiri lugha ya alama
Kampuni moja ya nchini Kenya inafanya juhudi za kutafsiri maneno kwenda katika lugha ya alama kwa kutumia picha za kielektroniki zinazofahamika kama Avatar. Ungana na Angela Mdungu katika makala ya Sema Uvume kufahamu zaidi.
Utata kuhusu kura ya mapema Zanzibar
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imesema, kura ya mapema itafanyika kama ilivyo kwenye sheria ya tume hiyo licha ya chama kikuu cha upinzani- ACT Wazalendo kupinga. Mohammed Khelef amezungumza na Ismail Jussa makamu mwenyekiti wa chama hicho kujua ni kwanini wanalipinga hilo.
Je dunia inafanya vya kutosha kulinda uhuru wa kuabudu?
Siku ya kumbukumbu ya waathirika wa ukatili wa kidini ni siku inayowakumbuka wale wote walioteseka, kujeruhiwa au kupoteza maisha kwasababu ya imani zao. Siku hii pia inaibua masuali mazito ya iwapo dunia inafanya juhudi za kutosha kulinda uhuru wa kuabudu. Mbiu ya Myonge inaangazia hilo, mtayarishaji ni Najjat Omar.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 1 wa 7
Ukurasa unaofuatia