1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maharamia waichia meli Somalia

24 Mei 2024

Maharamia waliokuwa wameiteka nyara meli moja ya kibiashara iliyokuwa umbali wa maili 420 kusini mashariki mwa pwani ya mji wa Merka nchini Somalia wameiachia huru na wahudumu wa meli hiyo wanaripotiwa wako salama.

https://p.dw.com/p/4gFkA
India Somalia uharamia
Baadhi ya maharamia waliowahi kukamatwa na jeshi la India katika bahari ya Somalia.Picha: Indian Navy/AP/picture alliance

Taarifa hizo zilitolewa siku ya Ijumaa (Mei 24) na Shirika la Uendeshaji Biashara la Uingereza (UKMTO) bila ya kutaja jina la meli hiyo. 

Hata hivyo, Kikosi cha Umoja wa Ulaya cha Kupambana na Ugaidi katika Bahari Hindi na Bahari ya Shamu kimesema watu wanaoshukiwa kuwa maharamia waliabiri meli ya kibiashara ya Basilisk yenye bendera ya Liberia katika eneo sawa na hilo siku ya Alhamisi (Mei 23).

Soma zaidi: Maharamia waiteka meli katika pwani ya Somalia

Umoja wa Ulaya ulisema kikosi chake kinachoendesha operesheni iitwayo Atlanta kilituma manuwari yake iliyokuwa karibu kukabiliana na tukio hilo.

Kati ya mwaka 2008 na 2018, maharamia wa Somalia walivuruga shughuli katika pwani ya taifa hilo.

Lakini kulikuwa kumeanza kupatikana utulivu hadi mwishoni mwa mwaka jana wakati matukio ya uharamia yaliripotiwa kuanza tena eneo hilo.