1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSomalia

Maharamia wa Somalia waiachia meli ya Bangladesh

Lilian Mtono
14 Aprili 2024

Maharamia nchini Somalia wameiachilia meli ya Bangladesh pamoja na mabaharia 23 wa meli hiyo baada ya kuishikilia kwa mwezi mmoja.

https://p.dw.com/p/4ejvP
Vikosi vya Somalia
Maafisa wa Polisi la Wanamaji wa Somalia PMPF wakishika doria katika Ghuba ya Aden karibu na pwani ya Jimbo la Puntland Picha: Jackson Njehia/AP Photo/picture alliance

Msemaji wa kampuni inayomiliki meli hiyo ya mizigo ya SR Shipping Limited Mizanul Islam amesema meli hiyo ya MV Abdullah iliondoka mapema jana Jumamosi katika pwani ya Somalia kuelekea Dubai.

Amesema mabaharia hao wana afya njema na kuongeza kuwa wanatarajia kufika Dubai Aprili 20, na kisha mabaharia hao watasafirishwa kwa ndege hadi Bangladesh.

Soma pia: Maharamia waiteka meli katika pwani ya Somalia

Maharamia hao waliikamata meli hiyo iliyokuwa imepakia makaa ya mawe katika Bahari ya Hindi Machi 12, ikiwa njiani kuelekea Dubai, kupitia Msumbiji na kuitaka kampuni hiyo kulipa kikomboleo ili kuiachia meli hiyo.

Hata hivyo kampuni hiyo haijazungumzia ikiwa ililipa kikomboleo hicho baada ya makubaliano ya kuiachia meli hiyo.