1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahamat Itno aapishwa kuwa rais wa Chad

24 Mei 2024

Aliyekuwa kiongozi wa kijeshi wa Chad, Mahamat Idriss Itno, ameapishwa rasmi kuwa rais kwa muhula wa miaka mitano kufuatia uchaguzi wa kwanza tangu aliporithi madaraka kutoka kwa baba yake, Idriss Deby Itno.

https://p.dw.com/p/4gEfd
Mahamat Idriss Deby wa Chad
Mahamat Idriss Deby Itno akiapishwa kuwa rais wa kipindi cha miaka mitano.Picha: MOUTA/dpa/picture alliance

Wiki iliyopita, Mahakama ya Kikatiba ya Chad ilimthibitisha Mahamat kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Mei 6, baada ya kupata asilimia 60 ya kura zilizopigwa.

Soma zaidi: Mahamat Idriss Deby Itno kuapishwa leo kama rais wa Chad

Mahamat, ambaye ni mwana wa kiume wa mtawala wa zamani wa Chad, Idriss Déby Itno, alinyakuwa madaraka pamoja na kundi la majenerali wengine wa kijeshi mnamo mwaka 2021 baada ya kifo cha baba yake na kisha akasitisha kutumika kwa katiba.

Soma zaidi: Deby ashinda uchaguzi mkuu Chad

Wakati anafariki dunia, baba yake alikuwa ameshaitawala nchi hiyo ya Ukanda wa Sahel kwa zaidi ya miaka 30.

Upinzani ulipinga matokeo ya uchaguzi huo ukidai kulikuwa na visa vya udanganyifu kwa kiwango kikubwa, lakini Mahakama ya Kikatiba ilipinga madai hayo.