1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChad

Mahamat Idriss Deby Itno kuapishwa leo kama rais wa Chad

23 Mei 2024

Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno, ambaye ameiongoza serikali ya Chad kwa muda wa miaka mitatu iliyopita, ataapishwa leo kama Rais wa nchi hiyo baada ya kushinda katika uchaguzi uliokabiliwa na upinzani mkali.

https://p.dw.com/p/4gCGS
Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno baada ya kupiga kura mjini N'Djamena
Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno baada ya kupiga kura mjini N'DjamenaPicha: Issouf Sanogo/AFP/Getty Images

Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno, ambaye ameiongoza serikali ya Chad kwa muda wa miaka mitatu iliyopita, ataapishwa leo kama Rais wa nchi hiyo baada ya kushinda katika uchaguzi uliokabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa vyama vya kisiasa vya upinzani nchini humo.

Kuapishwa kwa Deby, kunaashiria mwisho wa miaka mitatu ya utawala wa kijeshi katika nchi hiyo muhimu kwenye mapambano dhidi ya makundi ya kijihadi katika eneo la Sahel.

Soma pia: Mpinzani wa Deby ataka matokeo ya uchaguzi Chad yafutwe 

Sherehe hiyo ya kuapishwa pia inakifanya kuwa rasmi kile ambacho upinzani umelaani na kuita utawala wa kurithi wa familia au nasaba ya Deby.

Waziri Mkuu Succes Masra, mmoja wa wapinzani wakuu wa Deby kabla ya kuwa waziri mkuu, alijiuzulu jana baada ya kushindwa kwa chama chake katika uchaguzi huo baada ya kuwa uongozini kwa miezi minne tu.

Deby alishinda rasmi kwa asilimia 61 ya kura katika uchaguzi huo wa Mei 6 ambao mashirika ya kimataifa yasio ya kiserikali yameutaja kutokuwa huru wala kuaminika huku mpinzani wake mkuu akiuita wa"udanganyifu".