1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya Kenya yasimamisha ubinafsishaji

Sudi Mnette
5 Desemba 2023

Mahakama kuu nchini Kenya imesimamisha mpango kubinafsisha makampuni mengi ya serikali baada ya chama kikuu cha upinzani nchini humo kufungua kesi, kupinga mpango huo wa serikali wenye nia ya kuongeza mapato ya nchi.

https://p.dw.com/p/4ZnKi
William Ruto Kenia  Africa Climate Summit
Picha: Khalil Senosi/AP/picture alliance

Serikali ya Kenya iliyaorodhesha makampuni 35 kuwa katika mpango wa kubinafsishwa na wiki iliyopita makampuni 11 ikiwemo la mafuta na gesi na lile la uendeshaji shughuli za usafirishaji nishati, yalitangazwa rasmi kuwa katika mchakato wa kuuzwa. Hata hivyo chama kikuu cha upinzani kinachoongozwa na Raila Odinga kiliupinga uamuzi huo mahakamani kikitowa hoja kwamba, hatua ya kuuza makampuni hayo inapaswa kuamuliwa kupitia kura ya maoni kutokana na umuhimu wa kimkakati wa makampuni hayo. Jaji Chacha Mwita wa mahakama kuu jana jioni alitowa uamuzi wa kuusitisha mpango wa serikali akisema hatua hiyo imegusa masuala ya kikatiba na kisheria ambayo ni muhimu kwa umma wa Kenya. Kenya inakabiliwa na matatizo makubwa ikiwemo kupungukiwa na mapato pamoja na kuporomoka kwa thamani ya sarafu yake, mambo ambayo yameifanya  kuwaongezea mzigo wa matatizo ya kiuchumi wananchi wake.