1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama Kenya yaamuru Mackenzie kubakia rumande

10 Agosti 2023

Mahakama ya Shanzu mjini Mombasa, Kenya imeamuru kuendelea kushikiliwa mshukiwa wa mauaji ya Shakahola, Paul Mackenzie na wenzake kwa siku nyingine 47 kutokana na uzito wa maafa yaliyotokea Shakahola.

https://p.dw.com/p/4V14d
Vifo vilivyotokana na itikadi kali za kidini Kenya
Maafisa wa polisi wakibeba miili iliyofukuliwa kwenye msitu wa ShakaholaPicha: Stringer/AA/picture alliance

Hakimu Mkuu Yusuf Shikanda ameieleza Mahakama ya Shanzu kwamba ipo haja ya kuendelea kumzuia Mackenzie na wenzake hadi uchunguzi utakapokamilika.

Akiwa mahakamani leo Mackenzie alionekana mchangamfu, lakini alilalamika kupitia mateso huko rumande, akidai hali vizuri wala haogi.

Wakili wake Wycliff Makasembo, ameieleza mahakama kuwa maneno hayo yalikuwa mzaha tu, lakini ameonya kusitisha uchunguzi ikiwa maafisa wa polisi wataendelea kumnyanyasa, ikiwemo kuwakatalia mawakili wake kumtembelea rumande.

Mackenzie, mkewe Rhoda Maweu na washukiwa wengine wanakabiliwa na mashtaka 12 yakiwemo mauaji ya halaiki.