1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu waandamana Brussels kupinga ubanaji matumizi

30 Septemba 2010

Maelfu ya watu kutoka katika nchi za Umoja wa Ulaya wameandamana mjini Brussels Ubelgiji, kupinga mipango ya kubana matumizi iliyochukuliwa na serikali za nchi nyingi zinazo tumia sarafu ya euro

https://p.dw.com/p/PQFt
Waandamanaji mjini BrusselsPicha: AP

Brussels ndiko makao makuu ya Umoja wa Ulaya, ambapo polisi walilazimika kuyazingira makao hayo kuzuia waandamanaji.

Inakadiriwa kuwa kiasi ya watu laki moja walishiriki katika maandamano hayo hapo jana.Katibu Mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi barani Ulaya John Monks amesema kuwa wafanyakazi barani Ulaya wamekuwa wahanga wa kuyumba kwa uchumi kulikosababishwa na mabenki pamoja na walanguzi wa fedha.

Wakati huo huo mgomo wa saa 24 umeanza nchini Uhispania na kusababisha usumbufu mkubwa katika sekta ya usafiri wa umma, viwanda vya magari pamoja na sekta nyingine.

Mwandishi:Aboubakary Liongo