1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madrid na Barcelona wapepetwa

4 Oktoba 2021

Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti ni miongoni mwa makocha wanaopitia kipindi kigumu kwa sasa kwani katika mechi zao tatu zilizopita kwenye mashindano yote, miamba hao hawajatoa ushindi.

https://p.dw.com/p/41FGV
Champions League 2021 Real Madrid vs Sheriff Tiraspol
Picha: Action Plus/picture alliance

Masaibu yalianza mwishoni mwa wiki iliyopita katika La Liga walipotoka sare na Villareal kisha katikati ya wiki katika Champions League wakafungwa na FC Sheriff na hapo jana walitandikwa magoli mawili kwa moja na Espanyol.

Ancelotti akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya mechi hiyo alisema huo wa Jumapili ndio uliokuwa mchezo wake mbaya zaidi kuwahi kusimamia tangu achukue ukocha wa Madrid.

Kwengineko Ronald Koeman amefurahishwa na hatua ya Rais wa klabu ya Barcelona Joan Laporta ya kumuunga mkono hadharani licha ya klabu hiyo kupoteza mechi yao ya La Liga mjini Madrid walipokuwa wakipambana na Atletico Madrid.

Laporta alisema kwamba Koeman anastahili kupewa muda kabla kubadilisha matokeo ya timu hiyo na kuirudisha kuwa miongoni mwa timu mahiri zaidi Uhispania na barani Ulaya kwa ujumla.