1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADRID : ETA lajiandaa kwa mashambulizi mapya

6 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCd2

Hofu inaongezeka kwamba kundi la ETA linalotaka kujitenga kwa jimbo la Basque nchini Uhispania linajiandaa kuanzisha mashambulizi mapya ya mabomu nchini Uhispania.

Hali hiyo imekuja baada ya polisi kugunduwa vifurushi viwili vya kilo 80 ya mabomu karibu na mji wa Bilbao.Ugunduzi huo pia umekuja siku mbili baada ya polisi kugunduwa takriban kilo 100 za mabomu kwenye gari moja lililotelekezwa kwenye sehemu ya kuegeshea magari ya eneo hilo hilo.

ETA imedai kuhusika na mripuko wa bomu lililotegwa kwenye gari mwishoni mwa wiki iliopita katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Madrid ambao umeuwa mtu mmoja na kujeruhi wengine wengi na hiyo kuashiria kumalizika kwa usitishaji wa mapigano uliodumu kwa miezi tisa.