Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu na Shirikisho la Vyama vya Wafanyikazi Kenya imeingilia kati kusuluhisha mgogoro kati ya serikali na Chama cha Madaktari juu ya mgomo wa madaktari.
Viongozi wa chama cha madaktari wameepuka tena kifungo cha mwezi mmoja baada ya hukumu yao kuahirishwa mara ya tatu kwa muda wa siku saba kuruhusu mazungumzo kufanyika. Mgomo wa madaktari umeendelea kwa miezi miwili sasa.