1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madaktari 3 wakamatwa kwa mauaji ya daktari mwenzao DRC

Mohammed Khelef
8 Agosti 2019

Mwendesha mashtaka wa makahama ya kijeshi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema madaktari watatu wamekamatwa na wanazuiliwa kwa tuhuma za mauaji ya daktari mmoja wa Umoja wa Mataifa.

https://p.dw.com/p/3NYY6
BG Ebola-Ausbruch im Kongo
Picha: picture-alliance/dpa/G. Cloarec

Mwendesha mashtaka wa makahama ya kijeshi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema madaktari watatu wamekamatwa na wanazuiliwa kwa tuhuma za mauaji ya daktari mmoja wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ambaye alikuwa ni miongoni mwa madaktari wanaopambana na mripuko wa homa ya Ebola.

Daktari huyo raia wa Cameroon, Richard Valery Mouzoko Kiboung, aliuawa kwa kupigwa risasi mnamo Aprili 19 kwenye shambulio katika hospitali moja katika mji wa Butembo mashariki mwa Kongo.

Mwendesha mashtaka wa kijeshi katika jimbo la Kivu Kaskazini, Luteni-Kanali Jean-Baptiste Kumbu Ngoma, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba madaktari waliokamatwa watashtakiwa kwa makosa ya ugaidi na jinai na kwamba bado kuna daktari mmoja ambaye bado anatafutwa.