Machafuko Ugiriki | Magazetini | DW | 09.12.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Machafuko Ugiriki

Hali nchini ugiriki,Pakistan ni mada za wahariri leo.

Machafuko Ugiriki.

Machafuko Ugiriki.

Uchambuzi wa wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo, umegusia mada mbali mbali-kuanzia machafuko nchini Ugiriki;Ugaidi nchini Pakistan,hukumu ya polisi mjerumani juu ya kifo korokoroni cha marehemu Jalloh, mkimbizi kutoka Sierra Leone, hadi jinsi ya kupambana na maharamia wa kisomali.

Ramadhan Ali akiwakagulia leo safu hizo za wahariri anaanza na gazeti la OLDENBURGISCHE VOLKSZEITUNG linaloandika:

"Kile hasa kilichotokea mjini Athens (Ugiriki) jumamosi iliopita pale mtoto wa miaka 15 alipouliwa na risasi zilizofyatuliwa na polisi,kinapaswa kuchunguzwa wazi wazi na haraka.Serikali ya waziri mkuu-muhafidhina Konstantinos Karamanlis ina dhamana 3 za kutekeleza:

La kwanza ni la kiadilifu,la pili ,ni kuonesha hili ni dola linalofuata sheria na la tatu ni la kisiasa."

"Kuhusu jukumu la tatu ,Ugiriki, kimsingi ,inajikuta sasa katika hali ya hatari....na ni jambo la kufadhahisha kuona kifo cha mtoto wa miaka 15 kuongoza katika wimbi la machafuko nchini.

Wafuasi wa mrengo wa shoto wa Ugiriki wamekamia sasa kuasi kote nchini dhidi ya utawala wasioupenda.Ugiriki lakini,ni nchi ya demokrasi inayofanya kazi na kikosi cha polisi cha kidemokrasi."

Likichambua Pakistan na ugaidi, gazeti la Ha nnoversche Allgemeine Zeitung laandika:

"Hakuna nchi iliojipigia upatu ni mhimili wa maovu kwa aina alivyonadi rais George Bush kama Pakistan.Lakini, hakuna anaetaka kuitumbukiza Pakistan chungu kimoja na Korea ya Kaskazini au Iran.Miaka iliopita lakini,Pakistan hatua kwa hatua, imejitosa katika maovu ingawa ni mshirika wa Marekani.

Tayari wakati wa utawala wa Jamadari Musharraf,ilikuwa vigumu kuidhibiti nchi hii- tangu Kashmir hata jimbo linalopakana na Afghanistan,mbegu zilizooteshwa na Idara ya Usalama ya Pakistan miaka ya 1990 katika kupalilia wafiasi wenye itikadi kali ya kiislamu sasa zinachipuka."

Kuhusu hukumu ya polisi juu ya kifo gerezani cha mkimbizi wa Kisierra Leone -Jalloh,gazeti la Mitteldeutsche Zeitung laandika:

"Hakuna mkoa wowote wa Ujerumani ambako miaka michache iliopita, mashambulio ya wafuasi wenye siasa kali za mrengo wa kulia dhidi ya wageni au wenye mawazo mengine kama katika Sachsen-Anhalt.

Na baada ya kupita miaka mingi imedhihirika kunatokana na uzembe wa polisi huko wa kupambana barabara na wahalifu wa mrengo huo wa kulia.Imesadifu huko Dessau mkasa wa askari polisi umegonga vichwa vya habari nchini kote pale uchunguzi wa askari 3 dhidi ya wavunja sheria wa mrengo wa kulia kutiwa munda na makamo-rais wa Idara ya Polisi ya mji huo wa Dessau.Kubainika sasa mkasa wa Jalloh si kashfa ya kisheria tu,bali ni wa kiadilifu kwa askari alieshtakiwa kwa kutompa msaada marehemu kutokutikana na hatia."

Likitukamilishia uchambuzi huu kwa kisa cha maharamia wa kisomali katika pwani ya pembe ya Afrika,gazeti la Berliner Morgenpost laandika:

"Hata kwa kujizatiti zaidi kwa manuwari, hakutatosha pekee kukomesha uharamia pwani ya Afrika mashariki.Kwa kadiri maharamia hao waweza kukimbilia serikalini na katika nchi mfano wa Somalia isio na sheria, na hata kuwaajiri maharamia zaidi,vita vya baharini ni sehemu tu ya kupigania njia za usalama za misafara ya baharini...."