1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mabomu yaua watu kadhaa nchini Pakistan

Kalyango Siraj11 Machi 2008

20 wauawa na 165 kujeruhiwa

https://p.dw.com/p/DMVJ
Waokoaji na maafisa wa usalama wakusanyika katika makao makuu ya idara ya upelelezi mjini Lahore yaliyoshambuliwaPicha: AP

Takriban watu 20 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika milipuko miwili ya mabomu nchini Pakistan.

Hadi sasa hakuna kundi lililojitokeza kudai kuhusika na milipuko hiyo iliokuja baada ya wiki moja ambapo watu wawili wakujitolea mhanga walipojilipua katika kituo cha wanamaji mjini Lahore.

Milipuko yote miwili imetokea leojumanne katika mji wa Lahore.Milipuko hiyo ambayo imetokea dakika 15 baada ya mwingine ,polisi inasema ni kazi ya watu waliojitolea mhanga ambao wamefanya mashambulizi hayo kwa kujilipua.

Jengo la orofa saba ambalo ni makao makuu ya jeshi la polisi mjini humo ndio moja wa shabaha ya mashambulizi huku nyumba ambayo ni ofisi za kampuni inayotoa matangazo,ndio imeshambuliwa katika shambulio lingine.

Katika mashambulio yote mawili takriban watu 20 wameuawa na wengine zaidi ya 150 wamejeruhiwa.

Mkuu wa Polisi ya mji wa Lahore,Malik Mohammed Iqbal amenukuliwa akisema kuwa, mlipuko katika ofisi za kitengo cha polisi cha upelelezi mjini humo umesababishwa na gari ambalo lililokuwa limejaa na baruti kulipuka baada ya kusimamishwa katika eneo la maegesho la jengo hilo.Eneo lilikolipuka ni karibu na kitengo cha polisi kinachopambana dhidi ya ugaidi.

Afisa mwingine wa polisi-Pervez Malik -amenukuliwa akisema kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na mlipuko huo, katika ofisi za polisi, ni 15 na 165 wamejeruhiwa.

Mlipuko mwingine umesasambua ofisi za kampuni inayoshughulika na matangazo katika kiunga cha mji huo ambako ni sehemu ambako wanakoishi watu.Mtaa huo uko umbali wa kilomita 25 kutoka mlipuko mwingine ulioharibu jengo la polisi ulipotokea .Afisa wa mwingine wa polisi amesema kuwa waliouawa katika shambulio la pili ni watu watatu,wakiwemo watoto wawili wa mfanyakazi katika bustani za karibu.

Milipuko hii imekuja wiki moja baada ya kutokea shambulio la kujitoa mhanga ambapo mtu huyo alijilipua ndani mwa kituo cha shule ya jeshi la wanamaji mjini humo na kuwauwa watu watano na kuwajeruhi wengine 19.

Rais Perves Musharraf,ambae ni mshirika mkuu wa Marekani katika vita dhidi ya ugaidi wa kimataifa-amelaani shambulio hilo,akisema kuwa visa vya kigaidi havitaweza kuishawishi serikali kupoteza lengo lake katika vita dhidi ya ugaidi.

Mji wa Lahore ambao unakaribia mpaka wa nchi hiyo na India, umekuwa kidogo haujaathirika sana na ghasia zilizoikumba miji mingi ya Pakistan,ingawa ,mwezi wa januari lilishuhudia shambulio la kujitoa mhanga ambapo watu 20 waliuawa,wengi wao wakiwa askari polisi.

Pakistan imekuwa ikipambana dhidi ya ugaidi wa makundi ya kiislamu yenye msimamo mkali yakiongozwa na kundi la Al-Qaida pamoja na wapiganaji wa Kitaliban,tangu rais Musharraf alipojiunga na Marekani katiika kampeini dhidi ya ugaidi tangu mwaka wa 2001.Lakini ghasia nchini Pakistan zimekuwa zikiendelea tangu mwazo wa mwaka wa 2007.

Takriban watu 600 wameuawa tangu mwaka huu uanze katika mashambulizi kadhaa.Mingoni mwa mashambulio hayo ni yale ya kujitoa mhanga, mabomu ya kando mwa barabara,pamoja na mapigano mengi yakitokea katika mpaka wa Pakistan na Afghanistan huku mengine katika miji kadhaa.

Mashambulizi mengi yamelenga askari jeshi, polisi na vikosi vingine vya dola.

Mwanajeshi wa ngazi ya juu- wa cheo cha Luteni Generali-Mustaq Baig-wa kitengo cha utibabu cha jeshi la ulinzi la Pakistan ni miongoni mwa wahanga wa mashambulio ya kujitolea mhanga.

Alishambuliwa mjini Rawalpindi Febuari 25.

Mashambulio ya leo jumanne yanatia changamoto mpya kwa serikali inayotarajiwa ya taifa hilo ambalo ni mshirika mkuu wa Marekani.