1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

M23 yatangaza kujiondoa katika mji wa Uvira nchini Kongo

16 Desemba 2025

Kundi la waasi la M23 limetangaza leo kuwa limekubali ombi la Marekani la kujiondoa kutoka mji wa Uvira, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/55Raq
Kongo, Uvira 2025 | waasi wa M23
Wapiganaji wa M23 wakishika doria katika mji wa Uvira mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mnamo Desemba 12, 2025Picha: stringer/Xinhua/picture alliance

Kujiondoa kwa M23 Uvira kumethibitishwa kupitia taarifa iliyosainiwa na mratibu wa muungano unaojumuisha kundi hilo Corneil Nangaa.

M23 imetoa wito wa kuwekwa kwa mikakati ya kutosha kusimamia mji huo ikiwa ni pamoja na kuondoa wanajeshi, kuwalinda wakazi wa eneo hilo na miundombinu pamoja na kufuatilia makubaliano ya amani kwa kutoegemea upande wowote.

Kundi hilo pia linataka kutekelezwa kwa mapendekezo ya mpango wa amani yaliofikiwa katika mchakato sambamba wa amani wa mjini Doha nchini Qatar yaliyokubaliwa mwezi Novemba lakini ambayo hayajatekelezwa.

Pia limesema kujiondoa kwake Uvira ni ishara ya kujenga imani ili kutoa nafasi ya kufanikiwa kwa mchakato wa Doha