1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Brown akubali rasmi kumrithi Blair

18 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC15

Waziri wa fedha wa Uingereza Gordon Brown amekubali rasmi kuteuliwa kwake kama mrithi wa Tony Blair kukiongoza chama cha Labour.Brown alietoa tangazo hilo alipokutana na waandishi wa habari mjini London,atapokea wadhifa huo,Blair atakapoondoka kama kiongozi wa chama na waziri mkuu,mwishoni mwa mwezi Juni.Waziri Brown alithibitishwa kuwa kiongozi mpya wa chama hicho,baada ya mgombea mwingine pekee kushindwa kupata kiwango cha kura 45 zinazohitajiwa,kutoka kwa wabunge wengine wa Labour.