Ligi ya mabingwa barani Ulaya Liverpool dhidi ya Porto | Michezo | DW | 08.04.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Ligi ya mabingwa barani Ulaya Liverpool dhidi ya Porto

Ligi ya mabingwa awamu ya robo fainali inarejea uwanjani kesho Jumanne na Jumatano wakati Liverpool ya Uingereza ikitaka kurejea  ilichofanya msimu uliopita dhidi ya Porto kesho Jumanne.

Fußball | Champions League | Bayern München vs Liverpool | Hummels (imago/M. Koch)

Pambano la 16 bora la Champions League kati ya Liverpoll na Bayern Munich. Mo Salah akipambana na Mats Hummels wa bayern (kulia)

Ligi ya  mabingwa  awamu ya  robo  fainali inarejea  uwanjani kesho Jumanne  na  Jumatano  wakati Liverpool ya  Uingereza  ikitaka kurejea  ilichofanya  msimu  uliopita  dhidi  ya  Porto kesho Jumanne. Pia  kesho  Jumanne Tottenham Hot Spur inaikaribisha Manchester City  katika  uwanja  wao  mpya  wenye  uwezo  wa kuingiza  mashabiki 62,000  kaskazini  mwa  London.

Robo fainali ya  Champions  League imekuwa mwisho wa safari  ya Barcelona kwa misimu  mitatu mfululizo tangu  kunyakua  ubingwa wake  wa  tano wa  Ulaya mwaka  2015. Je  mara  hii  itavuka kikwazo dhidi  ya  Manchester United, jibu litapatikana  siku  ya Jumatano uwanjani Old Trafford. Ajax inatiana  kifuani  na  Juventus Turin siku  ya  Jumatano.

Afrika Fußball Champions League TP Mazembe - USM Algers (Getty Images/AFP/J. Kannah)

Kikosi cha TP Mazembe wakati huo wakiwa na Mbwana Samatta wa Tanzania (wa pili kutoka Kulia)

Barani Afrika awamu ya robo fainali  ya Champions League mkondo wa kwanza umemalizika na Simba SC  ambayo  inawakilisha  mataifa ya  Afrika  mashariki imeshindwa kutumia uwanja wa nyumbani  kwa kutoka  sare  ya bila  kufungana  na TP Mazembe ya DRC. Horoya ya Guinea ilitoka  sare  pia  na  Widad Casablanca ya Morocco, ambapo CS Contantine  ya  Algeria , ilipoteza  mchezo  wake nyumbani  dhidi  ya Esparance Tunis, ya Tunisia. Matokeo ambayo  yameshangaza  sana  ni  kati  ya  Mamelodi Sundowns ya Afrika  kusini  ilipoishindilia Al Ahly ya Misri  kwa  mabao 5-0 mjini  Johannesburg.

Afisa mtendaji mkuu  wa  Simba Crecentius Magori, alisema  shirikisho  la  kandanda  barani  Afrika umefanya  mabadiliko  ya  ghafla  ya  waamuzi wa  mchezo  wao  dhidi  ya  TP Mazembe na  kueleza  sababu zilizotajwa kuwa za kiufundi na shirikisho  hilo  la  kandanda  barani  Afrika CAF.