Lewandowski hafikirii kustaafu | Michezo | DW | 17.03.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Lewandowski hafikirii kustaafu

Mwanasoka bora wa mwaka duniani Robert Lewandowski amesema bado hana mawazo ya kutundika daluga. Amesema, huu si wakati wa kuchukua maamuzi kama hayo.

Mwanasoka bora wa mwaka duniani Robert Lewandowski amesema bado hana mawazo ya kutundika daluga na anaamini kwamba anaweza kubakia kwenye kiwango cha juu akiwa na kikosi chake cha Bundesliga kinachoongoza ligi kuu ya nchini Ujerumani.

Mshambuliaji huyo raia wa Poland ameliambia jarida la michezo la Bild la Ujerumani kwamba alikuwa anajua kwamba watu sasa wanaanza kupata wasiwasi kutokana na umri wake. Lewandowski ana miaka 32. Lakini hata hivyo amesema "Kusema kweli najisikia vizuri kuliko alivyokuwa na miaka 26 ama 27". Ameongeza kuwa "najiona kama mchezaji bora kabisa sasa kuliko miaka sita iliyopita". 

Lewandowski alikuwa ni mfungaji bora wa magoli katika kila mashindano ya msimu uliopita, wakati walipochukua ubingwa wa Bundesliga, na tena anaongoza orodha ya wafungaji bora katika Bundesliga msimu huu akiwa na mabao 32

Iwapo atashinda kwa kiwango cha goli moja kwa kila mechi 9 zilizosalia hadi msimu huu kukamilika, Lewandowski atakuwa amevunja rekodi ya mfungaji bora wa muda wote nchini Ujerumani Gerd Muller ya magoli 40 kati ya mwaka 1971-72.

Si rahisi kuamua ni kwa muda gani Lewandowski anaweza kuendeleza kasi aliyonayo. Yeye mwenyewe alisema, "Najiamini mwenyewe kwamba angalau nitakuwa katika kiwango hiki kwa muda mrefu ujao." Na haoni kama anataka kujiunga na ligi nyepesi kwa wakati huu, wakati akielekea ukingoni mwa kazi yake. Alisema "ninajiona nikihitimisha kucheza kandanda langu nikiwa na Bayern Munich, tena nikiwa katika kiwango cha juu." Lakini bado ni mapema mno kufanya hivyo," aliongeza.

Mashirika: DPAE