Leverkusen watakiweza kishindo cha Juventus? | Michezo | DW | 30.09.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Leverkusen watakiweza kishindo cha Juventus?

Ligi ya vilabu bingwa barani Ulaya inarudia mechi zake wiki hii ambapo Jumanne Bayer Leverkusen watakuwa wanawakaribisha mabingwa wa Italia Juventus katika uwanja wao wa nyumbani wa Bay Arena huko Leverkusen.

Bayern Munich wao wataelekea London kupambana na Tottenham Hotspur katika mechi ambayo huenda ikaamua nani atakayeliongoza kundi lao.

Mechi zengine za Jumanne zitawapatanisha Galatasaray na Paris Saint Germain halafu Real Madrid waminyane na Club Brugge ya Ubelgiji nao Manchester City wavaane na Lokomotiv Moscow uwanjani Etihad.

Baada ya kutoka sare ya kutofungana na Barcelona uwanjani Signal Iduna Park, wawakilishi wengine wa Ujerumani kwenye ligi hiyo Borussia Dortmund watakuwa wanaelekea ugenini kuzipiga na Slvaia Prague mechi hiyo ikichezwa Jumatano.

DW inapendekeza