1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leverkusen kutumia maumivu ya Ligi ya Uropa kushinda Pokal

25 Mei 2024

Bayer Liverkusen wanakutana na timu ya daraja la pili, Kaiserslautern baada ya kuangukia kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Atalanta ya Italia katika fainali ya kombe la Ulaya, Europa League.

https://p.dw.com/p/4gGsD
Ligi ya UEFA Uropa | Ademola Lookman
Mnigeria Ademola Lookman alipeleka kilio Leverkusen baada ya kupachika mabao yote matatu yaliopelekea timu yake ya Atalanta kubeba kombe la Ligi ya Uropa na kukatisha ndoto ya Leverkusen kushinda mataji matatu masimu huu.Picha: Hannah Mckay/REUTERS

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga, Bayer Leverkusen wanaendelea kuuguza maumivu ya kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Atalanta katika fainali ya Ligi ya Uropa siku ya Jumatano, lakini kocha Xabi Alonso amesema watatumia maumivu hayo kushinda Kombe la Ujerumani hii leo.

Ndoto ya Leverkusen ya kushinda mataji matatu msimu huu ilisambaratishwa na kipigo cha Atalanta, lakini bado wanaweza kupata mataji mawili ya kwanza ya ndani iwapo wataishinda Kaiserslautern mjini Berlin.

Kocha wa Kaiserslautern Friedhelm Funkel, amekiri kuwa watacheza dhidi ya moja ya timu bora zaidi barani Ulaya, lakini wanajifaharisha kufikia hatua hiyo.