Leipzig wakosa nafasi ya kuipiku Bayern uongozini | Michezo | DW | 10.02.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Leipzig wakosa nafasi ya kuipiku Bayern uongozini

Mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner alikosa nafasi ya wazi ya kufunga goli katika kipindi cha pili na kuiweka uongozini timu yake dhidi ya Bayern Munich katika mechi ya Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga.

Mechi hiyo ilichezwa Jumapili uwanjani Allianz Arena ambapo miamba hao wawili walitoka sare ya kutofungana.

Licha ya sare hiyo Bayern wanasalia kileleni mwa jedwali la Bundesliga wakiwa na pointi arubaini na tatu pointi moja nyuma ya Leipzig.

Borussia Dortmund ambao walizabwa magoli manne kwa matatu na Bayer Leverkusen hapo Jumamosi wanasalia kwenye nafasi ya tatu wakiwa na pointi thelathini na tisa sawa na Borussia Mönchengladbach wanaoishikilia nafasi ya nne halafu tano bora inafungwa na Bayer Leverkusen wenye alama thelathini na saba.

Kama ilivyo ada kila Jumamosi tunakutangazia mechi moja ya kusisimua na Jumamosi iliyopita ilikuwa ni mechi kati ya Hertha BSC Berlin na Mainz 05 tuliyokupeperushia.