Lebanon yatimiza miaka 76 ya uhuru | Matukio ya Kisiasa | DW | 22.11.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Lebanon yatimiza miaka 76 ya uhuru

Lebanon inaadhimisha miaka 76 ya uhuru wake huku raia wake wakisema huu ndio mwaka pekee ambao wanahisi kuwa na uhuru wa kweli.

Wanasiasa hao wameonekana kwa pamoja kwenye gwaride hilo kwa mara ya kwanza tangu kulipoanza maandamano makubwa ya kitaifa yaliyosababisha serikali ya waziri mkuu Saad al-Hariri kujiuzulu.

Rais wa Lebanon Michel Aounspika wa bunge na waziri mkuu huyo aliyejiuzulu walikaa pamoja chini ya hema ya wizara ya ulinzi. Gwaride ambalo hufanyika katikati ya mji wa Beirut hii leo halikufanyika kwa kuwa bado eneo hilo linakaliwa na waandamanaji, ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja tangu yalipoanza.

Rais Aoun alipotoa hotuba kwenye maadhimisho hayo ya uhuru amesisitiza kwamba huu sio muda wa kuzungumza na badala yake ni muda wa kufanya kazi. Amesema migongano ya kisiasa imeendelea kusababisha kucheleweshwa kuundwa kwa serikali mpya na kuongeza kwamba kunahitajia uangalifu mkubwa ili kuzuia hali kuwa mbaya zaidi.

"Ndugu zangu waLebanon, ninawahutubia huku nikitambua kwamba huu sio wakati wa hotuba na sherehe. Ni wakati wa kufanya kazi kwa bidii kwa sababu tunakimbizana na wakati. Serikali mpya iliyosubiriwa na Lebanon ilitakiwa kuwa imeanza kazi. Lakini, mizozo inayodhibiti siasa za Lebanon imetulazimisha kuwa waangalifu ili kujiepusha na hatari zaidi, na kupata serikali itakayokidhi matarajio ya wengi." alisema Aoun kwenye hotuba aliyoitoa kupitia televisheni.

Libanon Proteste Sitzblockade

Waandamanaji wameendelea kusalia kwenye baadhi ya maeneo hata wakati wa maadhimisho hayo.

Taifa hilo limekumbwa na maandamano makubwa tangu Oktoba 17 yanayoshinikiza mabadiliko makubwa ya serikali. Maandamano hayo yaliwakusanya pamoja watu kutoka madhehebu mbalimbali huku wakiwa na matumaini kwamba shinikizo hilo litauondoa mfumo ambao wanadai umeshindwa.

Hiyo ni mara ya kwanza kwa madhehebu tofauti nchini humo kuungana pamoja bila ya mwito kutoka chama cha siasa na kuvipinga vyama vyote, alisema mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu na kuongeza kuwa huo ndio uhuru na ulio dhahiri.

Novemba 23 mwaka 1943 Lebanon

Sikiliza sauti 60:00

03.11.2019 Matangazo ya jioni

ilipata uhuru wake baada ya miaka 23 ya utawala wa Ufaransa, kutokana na wimbi la maandamano yaliyowaleta pamoja Wakristo na Waislamu. Hata hivyo taifa hilo lilijikuta katika wakati mgumu lilipoingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kati ya mwaka 1975 hadi 1990.

Rais Aoun bado amerejelea mwito wake kwa raia wa kufanyika mazungumzo, akisema hiyo ndio njia pekee ya kuusuluhisha mzozo huo.

 

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com