Larijani: Iran ko tayari kujilinda kwa gharama yoyote
2 Machi 2026
Mkuu wa usalama wa Iran, Ali Larijani amesema kwamba Jamhuri hiyo ya Kiislamu itajilinda bila kujali gharama yoyote, katika siku ya tatu ya vita na Marekani na Israel. Larijani ambaye ni afisa aliye na nguvu katika Baraza Kuu la usalama wa Taifa nchini Iran, ametoa kauli hiyo kupitia chapisho la kwenye mtandao wa X, akisema kuwa watajilinda vikali na kuwafanya maadui wajutie makosa yao.
Afisa huyo aidha, aliongeza kwa kusema kwamba, tofauti na Washington, Jamhuri hiyo ya Kiislamu imejipanga kwa vita vya muda mrefu dhidi ya Marekani na Iran.
Wakati huo huo Shirika la Hilali Nyekundu la Iran, limetangaza kwamba watu wasiopungua 555 wameuawa kufuatia mashambulizi ya pamoja ya Israel na Marekani. Shirika hilo la misaada, linadai kwamba zaidi ya wafanyakazi 100,000 wa uokoaji wamesambazwa nchi nzima na mikoa zaidi ya 130 imeathirika na vita.