LAGOS: Wanamgambo wawaua wanajeshi tisa | Habari za Ulimwengu | DW | 05.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LAGOS: Wanamgambo wawaua wanajeshi tisa

Kundi la wanamgambo nchini Nigeria limesema limewauwa wanajeshi tisa na kuziteka nyara boti mbili za jeshi wakati wa mapigano makali na vikosi vya wanajeshi katika eneo la mashariki la Niger Delta.

Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa ya kuthibitisha ripoti hiyo.

Katika barua pepe kwa vyombo vya habari, kundi la kupigania raslimali za Niger Delta, limesema linawatuma wapiganaji wake kwenda jimbo la Rivers kuanza kile ilichokiita mashambulio kadhaa ya makusudi dhidi ya viwanda vya mafuta.

Kufikia sasa, wafanyakazi saba wa kigeni waliotekwa nyara karibu na kituo cha kampuni ya mafuta ya ExxoMobil juzi Jumanne, hawajulikani waliko.

Wanamgambo wamewaachilia huru wafanyakazi wote 25 wa kampuni ya Royal Dutch Shell waliotekwa nyara mnamo Jumatatu wiki hii.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com