LAGOS : Obasanjo apima UKIMWI | Habari za Ulimwengu | DW | 02.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LAGOS : Obasanjo apima UKIMWI

Rais Olesegun Obasanjo wa Nigeria mwenye umri wa miaka 69 hapo jana amepima kwa hiari virusi vya HIV na UKIMWI mjini Abuja katika hatua ya kutaka kuwashajiisha wananchi wa Nigeria kuiga mfano huo.

Lakini kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Nigeria matokeo ya vipimo hivyo vilivyochukuliwa kama sehemu ya Siku ya UKIMWI duniani yatajulishwa kwa kiongozi huyo pekee.

Nigeria ambalo ni taifa lenye idadi kubwa kabisa ya watu Barani Afrika wakiwa milioni 130 lina watu milioni nne na nusu wenye virusi vya HIV.

Obasanjo amesema amezinduwa mpango wa Taifa wa Ushauri na Kupima ambao utawawezesha watu wengi kuwa na nafasi ya kupata huduma za jinsi ya kupambana na janga hilo la virusi vya HIV na UKIMWI.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com