1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUhispania

Uhispania yaahidi kuipa Ukraine mifumo ya kujilinda angani

27 Mei 2024

Uhispania imemuahidi Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mifumo ya kujilinda angani ili kusaidia katika mapambano dhidi ya karibu mabomu elfu 3 ambayo Zelensky amesema Urusi huyarusha nchini mwake kila mwezi.

https://p.dw.com/p/4gLUH
Madrid Uhispania | Pedro Sanchez na Volodymyr Zelensky
Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine akiwa na Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez aliyemuahidi kumpatia mifumo ya kujilinda angani Picha: Oscar del Pozo/AFP

Uhispania leo imemuahidi Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mifumo ya kujilinda angani ili kusaidia katika mapambano dhidi ya karibu mabomu elfu 3 aliyosema kwamba Urusi huyarusha nchini Ukraine kila mwezi, wakati vita hivyo vikiwa vimeingia mwaka wake wa tatu.

Zelensky na Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez wamesaini makubaliano ya usalama ya mataifa mawili yanayojumuisha yuro bilioni moja ya msaada wa kijeshi kwa Ukraine mwaka huu na yuro bilioni 5 ifikapo mwaka 2027.

Haya yanafanyika wakati Urusi imelaani hatua ya Katibu Mkuu wa NATO kutaka wanachama wa jumuiya hiyo ya kujihami kuiruhusu Ukraine kushambulia ndani ya Urusi kwa kutumia silaha za nchi za Magharibi.

Alipoulizwa iwapo NATO inakaribia makabiliano ya moja kwa moja na Urusi, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema jumuiya hiyo tayari inakabiliana na Urusi moja kwa moja.