1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAmerika ya Kaskazini

Korti ya juu Marekani yakataa kumkinga mshauri wa Trump

19 Machi 2024

Mahakama ya Juu ya Marekani hapo jana imekataa ombi la msaidizi wa zamani wa Donald Trump, Peter Navarro, kuepuka gereza wakati akikata rufaa dhidi ya kifungo cha kosa la kulidharau bunge.

https://p.dw.com/p/4dsiY
Washington, Marekani | Donald Trump na Peter Navarro
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akiwa na aliekuwa mshauri wake masuala ya biashara Peter NavarroPicha: Tasos Katopodis/Getty Images

Hii ni baada ya kukaidi wito wa kamati iliyochunguza shambulio la mwaka 2021 dhidi ya bunge. Navarro, ambaye alihudumu kama mashauri wa biahsara wakati wa utawala wa Trump, alipaswa kuripoti gerezani kutumikia kifungo cha miezi minne kulingana na wakili wake. 

Jaji Mkuu John Roberts, anaeshughulikia baadhi ya masuala ya dharura yanayohusisha kesi kutoka Washington DC, alikataa ombi la Navarro kwa niaba ya mahakama kuu. 

Soma pia:Mshauri wa zamani wa Trump Navarro aamriwa kuripoti gerezani

Kamati ya majaji ilimtia hatiani Navarro Septemba mwaka jana kwa kukaidi bunge baada ya kugoma kuitikia wito wa kamati iliyokuwa inaongozwa na Wademokratiki, ikichunguza shambulizi la Januari 6, ambapo wafuasi wa Trump walivamia bunge kujaribu kuzuwia uidhinishaji wa ushindi wa rais Joe Biden.