1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kipchoge ashinda mbio za London Marathon

28 Aprili 2019

Mkenya Eliud Kipchoge ameshinda London Marathon kwa mara ya nne mfululizo huku Muingereza Mo Farah aliyetarajiwa kutoa ushindani mkali akimaliza katika nafasi ya tano.

https://p.dw.com/p/3HZwo
BdTD Berlin Marathon
Picha: Reuters/F. Bensch

Mkenya Eliud Kipchoge ameshinda London Marathon kwa mara ya nne mfululizo huku Muingereza Mo Farah aliyetarajiwa kutoa 

Kipchoge ambaye alivunja rekodi ya dunia ya mbio za marathonn mjini Berlin mwaka jana, alikamilisha mbio za leo kwa muda wa saa mbili dakika mbili na sekunde thalathini na nane (2: 02: 38.)

Waethiopia Mosinet Geremew na Mule Wasihun walimaliza katika nafasi ya pili na ya tatu nyuma ya Kipchoge, ambaye alishindwa kuvunja rekodi yake mwenyewe ya Dunia kwa sekunde 59. Farah alimaliza mbio hizo kwa dakika 3 na sekunde moja nyuma ya Kipchoge, huku Muingereza Callum Hawkins akimaliza katika nafasi ya 10.

Kwa upande wa wanawake, Mkenya Brigid Kosgei, 25, alishinda mbio hizo na kuwa mwanamke wa kwanza mwenye umri mdogo kushinda London Marathon kwa wanawake. Mkenya mwingine Vivian Cheruiyot ambaye alishinda mbio za mwaka jana, alimaliza wa pili mbele ya Muethiopia Roza Dereje.