1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Kiongozi wa Hamas kufanya mazungumzo na Rais wa Uturuki

Tatu Karema
20 Aprili 2024

Kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh, anatarajiwa kukutana leo na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki, huku wasiwasi kuhusu mzozo katika eneo la Mashariki ya Kati ukiongezeka

https://p.dw.com/p/4f0Lg
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akihutubia wananchi kwakati wa mkutano wa hadhara katika uwanja wa ndege wa Ataturk mjini Istanbul, Machi 24,2024
Rais wa Uturuki Recep Tayyip ErdoganPicha: Serhat Cagdas/AA/picture alliance

Alipohojiwa jana na waandishi habari kuhusu ajenda ya mkutano wake na kiongozi huyo wa Hamas, Erdogan alisema ajenda hiyo itabaki kuwa kati yao wawili.

Juhudi za Erdogan za kuwa mpatanishi katika mzozo huo wa Palestina hazijafanikiwa hadi sasa.

Erdogan ameapa kusimama na Palestina 

Lakini baada ya Qatar kusema kuwa ingelifanyia tathmini jukumu lake kama mpatanishi kati ya Hamas na Israel, siku ya Jumatano, Erdogan alimtuma waziri wake wa mambo ya nje, Hakan Fidan, kwenda mjini Doha kama ishara mpya kwamba analitaka jukumu hilo.

Erdogan amedai kuwa angeliendelea kuitetea Palestina na raia wake wanaokandamizwa hata kama atabakia peke yake.