1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi mkuu wa Iran kulinda uwezo wa nyuklia na makombora

1 Mei 2026

Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Mojtaba Khamenei, ameapa jana kuwa atalinda uwezo wa nyuklia na makombora wa Jamhuri hiyo ya Kiislamu, ambayo Rais wa Marekani Donald Trump ametaka kukatiza kupitia mashambulizi ya anga.

https://p.dw.com/p/5D7Tj
Iran Tehran 2024 |  Ayatollah Mojtaba Khamenei
Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Mojtaba KhameneiPicha: Hamed Jafarnejad/ISNA/WANA/REUTERS

Katika taarifa iliyosomwa na mtangazaji wa televisheni ya serikali, Khamenei alisema sehemu pekee ya Wamarekani katika Ghuba ya Uajemi ni "chini ya maji yake" na kwamba "sura mpya" inaandikwa katika historia ya eneo hilo.

Khamenei ameongeza kusema kuwa Wairani milioni tisini ndani na nje ya nchi wanachukulia uwezo wote wa Iran wa utambulisho, kiroho, kibinadamu, kisayansi, kiviwanda na kiteknolojia kutoka teknolojia ya nano na teknolojia ya viumbe hai hadi uwezo wa nyuklia na makombora kuwa wa kitaifa.

Khamenei hajaonekana hadharani tangu achukue wadhifa wa kiongozi mkuu kufuatia kuuawa kwa babake katika mashambulizi ya anga ya mwanzo ya vita nchini humo.