KINSHASA : Mahkama yashika moto | Habari za Ulimwengu | DW | 21.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KINSHASA : Mahkama yashika moto

Mahkama Kuu ya Kinshasa imeshika moto leo hii huku kukiwa na mapigano ya mitaani ambayo yamezuka wakati kesi ya madai ya hujuma katika uchaguzi wa rais nchini humo ikianza kusikilizwa.

Milio ya risasi nje ya mahkama hiyo ilitibuwa mchakato wa kesi hiyo na iliendelea kwa dakika 45 wakati vikosi vya Umoja wa Mataifa vikiwasili na magari ya deraya na watu kukimbizana kutafuta hifadhi.

Kulikuwepo na mapigano kadhaa miongoni mwa watu 200 waliojitokeza kumuunga mkono Jan Piere Bemba mpinzani wa Rais Kabila ambaye anadai uchaguzi huo umehujumiwa.

Ofisi sita hadi saba za jengo hilo la mahkama la ghorofa mbili zilikuwa zikiwaka moto pamoja na samani na nyaraka ziliokuwemo ndani.

Askari wa Umoja wa Mataifa waliwahamisha watu waliokuwemo ndani ya ofisi hizo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com