KINGSTON: Kimbunga Dean chaelekea Mexico | Habari za Ulimwengu | DW | 20.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KINGSTON: Kimbunga Dean chaelekea Mexico

Kimbunga Dean kinaelekea Mexico leo, baada ya kuilazimisha Jamaica kutangaza hali ya tahadhari.

Kimbunga hicho kiliharibu nyaya za umeme, mapaa ya nyumba na kufunga barabara kwa takataka na miti iliyoanguka nchini humo. Maelfu ya watu hawana umeme kutokana na kimbunga hicho.

Waziri mkuu wa Jamaica, Portia Simpson Miller, alitangaza jana kwamba maafisa wa usalama watapewa mamlaka zaidi baada ya polisi kuripoti visa vya wizi wa mali katika kisiwa hicho cha Karibik.

Hali ya tahadhari nchini Jamaica ilitarajiwa kujadiliwa tena kwenye kikao cha baraza la mawaziri leo, lakini inatarajiwa hali hiyo kuendelea kwa kipindi cha mwezi mmoja ujao.

Waziri mkuu wa Jamaica ameonya kuwa uchaguzi uliopangwa kufanyika tarehe 27 mwezi huu nchini humo huenda ukaaharishwa kutokana na janga la kimbunga cha Dean.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com