1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kikosi cha Ulaya Ukanda wa Sahel chatakiwa kuondoka Niger

John Juma
1 Machi 2024

Kikosi cha Umoja wa Ulaya kinachojihusisha na usimamizi na utatuzi wa mizozo kwenye Ukanda wa Sahel (EUCAP) kimetakiwa kuondoka mara moja nchini Niger, moja ya mataifa yaliyo chini ya utawala wa kijeshi Afrika Magharibi.

https://p.dw.com/p/4d4Nr
Niger | Antje Pittelkau | Polisi EUCAP
Kiongozi wa kikosi cha EUCAP nchini Niger, Antje Pittelkau, akizungumza na maafisa wa kijeshi wa nchi hiyo mwezi Agosti 2021.Picha: Marou Madougou Issa/DW

Msemaji wa Umoja wa Ulaya aliliambia hayo shirika la habari la Ujerumani (dpa) mjini Brussels kwamba Umoja huo umelazimishwa kuharakisha mchakato wa kukiondoa kikosi cha EUCAP. 

Soma zaidi: Jumuiya ya ECOWAS yaiondolea Niger baadhi ya vikwazo

Mnamo mwezi Disemba, utawala wa kijeshi wa Niger uliamua kufuta ushirikiano na makundi mawili ya Umoja wa Ulaya, likiwemo hilo la EUCAP Sahel Niger na EUMPH, ambalo ni la ushirikiano wa kijeshi.

Wiki iliyopita, Umoja wa Ulaya ulilaani vikali shambulizi dhidi ya makao makuu ya kikosi cha EUCAP mjini Niamey, ambapo vifaa vya kikosi hicho viliporwa.

Kikosi hicho chenye takribani wanajeshi 130 kilikusudiwa kusaida katika vita dhidi ya ugaidi katika Ukanda wa Sahel.