Kifo cha Vitaly Churkin balozi wa Umoja wa Mataifa | NRS-Import | DW | 21.02.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

NRS-Import

Kifo cha Vitaly Churkin balozi wa Umoja wa Mataifa

Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Vitaly Churkin alifariki ghafla mjini New York Jumatatu . Balozi huyo alikuwa akijisikia vibaya alipokuwa ofisini kwake.

Russischer UN-Botschafter Witali Iwanowitsch Tschurkin (picture-alliance/Photoshot)

Balozi wa Urusi ndani ya Umoja wa Mataifa Vitaly Churkin

Churkin aliyebobea katika maswala ya demokrasia ya nchi za magharibi alipelekwa hospitali, ambako alifariki siku hiyo hiyo , siku moja tu kabla ya kutimiza miaka 65.

Watu wengi hususan viongozi wa nchi mbalimbali na  wajumbe wa Umoja wa mataifa wamekuwa wakiomboleza kifo cha balozi Churkin.

Churkin alikuwa mjumbe wa Urusi wa Umoja wa mataifa kuanzia 2006 na  mjumbe wa muda mrefu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa .

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Antonio Guterres alimpongeza Churkin na kusema kuwa alikuwa ni mwana diplomasia aliyebobea. "Balozi Churkin alitumikia wizara ya mamabo ya njee ya Urusi kwa njia nzuri na ya kipekee alipokuwa akipambana na migogoro migumu na mirefu ya historia ya hivi karibuni." Alisema Guterres

New York UN Generalsekretär Antonio Guterres (Reuters/S. Keith)

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Antonio Guterres

 

Pia raisi wa Urusi Vladimir Putin alimpongeza Churkin kwa kipaji chake na ujuzi na utaalamu aliokuwa nao.

Wanadiplomasia kutoka sehemu mbalimbali waliomboleza kwa kusema kuwa Churkin alikuwa bigwa katika kazi yake na pia  alikuwa ni mtu aliyekuwa akipenda kazi yake pamoja na   kutekeleza majuku majukumu yake .  Churkin alikuwa pia ni msomi aliyebobea  na alikuwa na shahada ya  juu  ya PHD katika  somo la   historia, lakini pia utotoni alikuwa ni muugizaji mzuri  wa kuchekesha.

Churkin akumbukwa na wengi

Samantha Power aliyekuwa balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa  chini ya utawala wa Barack Obama  aliandika  katika  mtandao wa kijamii wa twitter na kusema kuwa  Churkin alikuwa mtu aliyebobea  "kidplomasia na  aliyejali sana sana  watu".  Aliendelea kuandika  kuwa Churkin alijaribu wakati wote kusawazisha mivutano baina ya Marekani na Urusi kwa kadiri ya uwezo wake.

Kifo cha Churkin kimetokea  katika wiki ambazo Urusi inajipanga na mkutano wa  Umoja wa mataifa na jumuiya ya kimataifa, pia wakati huo huo uteulewa mpya wa viongozi  mbalimbali katika ikula ya White house na juu ya hayo pia kuna mazungumzo ya Syria na Urusi.

 Balozi wa Uingereza ndani ya umoja wa mataifa , Matthew Rycroft alimwita  Churkin kuwa ni "gwiji  la wadiplomasia  na mtu mwenye tabia nzuri."

Churkin alijitokeza kuwa sura mpya katika masuala  ya wizara ya nje hapo mwaka 1986 enzi za Urusi ya zamani  ilipokuwa bado muungano ikiitwa Jamhuri za  Kisovieti, alipotoa ushahidi dhidi ya Marekani.

New York Sicherheitsrat Votum für neuen UN Generalsekretär Antonio Guterres (picture-alliance/AP Photo/United Nations Video)

Vitaly Churkin

Churkin pia aliwahi kuwa balozi wa Ubelgiji na Canada.

Katika mahojiano na  kituo cha matangazo ya televisheni cha  na RussiaToday Churkin alisema kuwa diplomasia siku hizi imekuwa ni "kazi ngumu" huku migogoro ya kisiasa ikiendelea na  wakati huohuo kukiwa na  hali ya utulivu.

 

Mwandishi :   Najma Said/APE

Mhariri :         Mohammed Abdul-Rahman

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com