1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Khartoum. Sudan yakana kutoa onyo.

7 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5I

Serikali ya Sudan imekana kutoa onyo kwa mataifa ya Afrika na Kiarabu kutotuma wanajeshi wa kulinda amani katika jimbo la Darfur.

Barua iliyotumwa na ubalozi wa Sudan katika umoja wa mataifa imesema kuwa kuchangia katika jeshi la umoja wa mataifa kutaonekana kama hatua ya kupambana na Sudan.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Sudan Lam Akol amesema barua hiyo haiwakilishi mawazo ya serikali.

Umoja wa mataifa unataka kuweka jeshi litakalokuwa na wanajeshi 20,000 , ili kusitisha mzozo katika jimbo la Darfur lakini Sudan inasema kuwa jeshi la umoja wa mataifa litakuwa ni kisingizio cha mataifa ya magharibi kuivamia nchi hiyo.

Marekani imeitisha kikao cha dharura kuhusiana na barua hiyo , ikiita kuwa ni changamoto ya moja kwa moja dhidi ya baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Jeshi la umoja wa Afrika lenye wanajeshi 7,000 limeshindwa kusitisha mzozo huo, ambapo watu wapatao 200,000 wameuwawa na zaidi ya milioni 2 wamekimbia makaazi yao.