Kenya yazindua reli nyingine ya SGR kupunguza msongamano | Matukio ya Afrika | DW | 16.10.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Kenya yazindua reli nyingine ya SGR kupunguza msongamano

Rais Uhuru Kenyatta amezindua mradi wa reli ya kisasa maarufu SGR utakaounganisha uwanja wa Kimataifa wa Jommo Kenyatta hadi jijini Nairobi. Reli hiyo itapunguza msongamano mkubwa wa magari na kugharimu dola milioni 6.

Barabara hiyo ya moja kwa moja ni sehemu ya mpango wa serikali wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Nairobi,  ambalo idadi ya watumiaji wa magari inazidi kuongezeka.

Benki ya Dunia ilikisia kuwa taifa hupoteza kima cha dola elfu tano kila siku kutokana na misongamano ya magari huku watu wakipoteza muda wao kwenye misongamano hiyo.

Msongamano wa magari pia huchangia wasafiri kukosa safari zao za ndege katika uwanja huu wa kimataifa wa Jommo Kenyatta. Rais Uhuru Kenyatta akizindua mradi huu baada ya benki ya dunia kujiondoa kwenye ubia na serikali ya Kenya alisema.

"Wengine wanasema ooh! hii reli inaenda wapi? hakuna kitu kibaya kama ujinga wa mtu ambaye fikra zake ni namna hii. Sasa sisi tukisema tunajenga hii kusaidia wananchi tatizo iko wapi?", alisema Kenyatta. 

Mradi huu ni matokeo ya ziara ya rais Kenyatta mwezi septemba mwaka uliopita katika taifa la China, kwenye kongamano lililowaleta pamoja viongozi wa Afrika pamoja na wawekezaji.

 SGR Express (DW/S. Wasilwa)

Kituo cha SGR

Mradi huu utatekelezwa na kampuni ya ujenzi wa barabara na madaraja ya China, kwa ushirikiano na serikali ya Kenya na mashirika ya kibinafsi.

Inakadirikwa kuwa magari elfu 60 hutumia barabara hiyo kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jommo Kenyatta hadi Westlands kila siku.

Barabara yenyewe ikikamilika idadi ya watumiaji magari itaongezeka kwa magari 25,000. Barabara yenyewe itakuwa na urefu wa kilomita 17. Badala ya kuchukua saa nyingi kufika uwanja wa kimataifa, barabara hiyo itakapokamilika mtumiaji atatumia dakika 10 au 15 kutoka katikakati ya jiji.

Hata hivyo wataalam wanasema kuwa mradi huu ni ghali mno ikilinganishwa na gharama inayostihili kuchukuliwa huku ushirikiano kati ya China na Afrika ukiendelea kupanuka.

 

DW inapendekeza