1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yatangaza sheria mpya ya uagizaji magari kutokea nje

Bruce Amani
8 Desemba 2021

Kenya imetangaza kuwa kuanzia Januari mosi mwaka 2022, waagizaji wa magari kutokea nje na wauzaji watalazimika kufuata sheria mpya.

https://p.dw.com/p/43z9W
Afrika Gebrauchtwagen Autohandel Autoverkauf
Picha: Yasuyoshi Chiba/Getty Images

Magari yaliyosajiliwa kwa mara ya kwanza kabla ya mwaka 2014 yamepigwa marufuku kuingia ndani ya mipaka ya Kenya ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Kulingana na notisi ya umma, mkurugenzi mkuu wa idara ya ubora wa bidhaa nchini Kenya, KEBS, Bernard Njiraini,magari yanayoendeshwa kwa upande wa kulia ambayo yalisajiliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015 na baadaye, ndio pekee yatakayoruhusiwa kuagizwa kutokea nje.

Kwa upande wake Jumuiya ya Afrika Mashariki ina mkakati na azma ya kushajiisha utengezaji wa magari ndani ya kanda hiyo inaisukuma hoja ya kupiga marufuku uagizaji wa magari yaliyotumika.