1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yatakiwa kushughulikia sakata la ardhi

Josephat Nyiro Charo8 Agosti 2014

Waziri wa ardhi wa Kenya anaendelea na mchakato wa kuzifuta hati za kumiliki ardhi zilizotolewa kwa makampuni na watu binafsi katika kaunti ya Lamu.

https://p.dw.com/p/1CrIG
Insel Lamu Kenia
Picha: Tony Karumba/AFP/Getty Images

Asasi ya kiraia inayoshughulikia mageuzi katika masuala ya umikili wa ardhi nchini Kenya, Kenya Land Alliance, inaitolea mwito serikali ya Kenya ichukue hatua madhubuti kulitatua tatizo la ardhi nchini humo kwa kuwa limekuwa jinamizi la kihistoria ambalo limesababisha chuki na hali ya kutoelewa hususan katika maeneo ambako wenyeji hawajatendewa haki kuhusu masuala ya ardhi.

Kwa wakati huu mjadala unaendelea huku waziri wa masuala ya Ardhi wa nchi hiyo, Charity Ngilu, akiendelea na mchakato wa kufutilia mbali hati za kumiliki ardhi za makampuni na watu waliojipatia ardhi kubwa ya kiasi cha 500,000 katika kaunti ya Lamu katika pwani ya Kenya, kwa njia isiyo halali. Agizo hilo lilitolewa na rais Uhuru Kenyatta, kufuatia kile kinachoonekana kuwa kashfa kubwa ya ardhi kuwahi kutokea katika historia ya Kenya.

Josephat Charo amezungumza na Odenda Lumumba, Mratibu wa Kitaifa wa asasi hiyo na kwanza anaelezea mtizamo wake kuhusu sakata hili linaloendelea.

Mwandishi: Josephat Charo

Mhariri: Saumu Yusuf