1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yarejesha sherehe za siku ya Moi

10 Oktoba 2018

Kenya imeanza tena kuiadhimisha siku ya Moi kama siku ya mapumziko baada kuwekwa kando kwa miaka saba. Hatua hii inafuatia uamuzi wa mahakama kuirejesha siku hiyo. Sophia Chinyezi amezungumza na mchambuzi wa masuala ya kisiasa Profesa Mohammed Manyora, kuhusu hatua hiyo.

https://p.dw.com/p/36Gwa

Serikali ya Kenya imeitangaza Oktoba 10 kuwa siku ya mapumziko. Hatua hii inafuatia shauri lililofunguliwa mahakamani na mwanasheria Gragory Nyauchi mwaka uliopita akihoji kufutwa kwa siku ya Moi kama siku inayoadhimishwa kitaifa. Nyauchi alisema alifanya hivyo ili kurekebisha upotoshaji wa katiba.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari siku ya Jumatatu, waziri wa mambo y ndani wa Kenya Fred Matiang'i alisema siku hiyo itaadhimishwa kutokana na amri ya mahakama, lakini akaongeza kuwa hakuna hasara itayotokea ikiwa itawekwa kando kwa sababu hata katiba haiitambui kama siku ya kitaifa.

Waziri Matiang'i alisema kama taifa linaloinukia kiuchumi, Wakenya wanahitaji kuutumia muda wao vizuri... na hii inaweza kuwa mojawapo ya sababu zilizozingatiwa katika kupunguzwa siku za sherehe za kitaifa kupitia marekebisho ya kikatiba.

Kenia ehemaliger Präsident Daniel arap Moi
Rais mstafu wa Kenya Daniel Arap MoiPicha: AP

Hukumu ya mahaka mwaka uliopita iliagiza kwamba Oktoba 10 itangazwe kuwa siku ya mapumziko ya kitaifa. Hata hivyo haikuwa wazi namna siku ya Moi itakaposherehekewa kwa vile haitambuliwi kikatiba kama siku ya kitaifa.

Katika hukumu yake Novemba 8, 2018, Jaji George Odunga aliamua kwamba kufuta kwa siku ya Mosi kulifanyika kinyume na sheria. Siku hii inanuwiwa kumuwezi rais wa zamani Daniel Moi.

Katika hukumu hiyo, mahakama ilielezwa kwamba kuondolewa kwa siku ya Moi kuwanyima Wakenya haki yao ya kuwa na siku ya mapumziko. Wakenya wataendelea kuadhimisha siku hiyo hadi pale bunge litakapobadili sheria na kuifuta au waziri wa mambo ya ndani aibadilishe na sherehe nyingine.

Kenya ina jumla ya siku 12 za kitaifa, tano kati ya hizo zikiwa za kidini. Siku moja ya mapumziko, ambayo ni Mei Mosi au siku ya Wafanyakazi, imewekwa kuwaenzi wafanyakazi katika sekta mbalimbali.

Mwandishi: Iddi Ssessanga
Mhariri: Sudi Mnette