Kenya yang′aa katika riadha Doha | Michezo | DW | 07.10.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Kenya yang'aa katika riadha Doha

Yale mashindano ya dunia ya riadha yaliyokuwa yanaendelea Doha Qatar yalikamilika Jumapili huku Marekani ikiongoza katika nafasi ya kwanza ikiwa na jumla ya medali ishirini na tisa.

Kenya wameiwakilisha Afrika vyema kwa kuinyakua nafasi ya pili wakiwa na jumla ya medali kumi na moja, tano kati ya hizo zikiwa dhahabu.

Rais wa Shirikisho la Riadha Duniani IAAF Sebastian Coe amesema kulikuwa na ufanisi mkubwa.

"Hatujakabiliana na visa vyovyote vibaya, wanariadha walikuja kwenye mashindano haya wakifahamu changamoto zitakazokuwa na kwa sehemu kubwa nafikiri wameshindana vyema sana," alisema Coe.

Uwanja uliotumika kwa mashindano hayo wa Khalifa kwa wakati mwengine ulikuwa hauna mashabiki ingawa makamu wa rais wa kamati andalizi ya mashindano hayo Dahlan Al-Hamad amesema hilo ni jambo la kawaida.

"Kujaza uwanja ni changamoto kwa kila mtu. Tumeiona changamoto hii si katika mashindano haya tu, ni katika karibu mashindano yote. lakini tunafurahia kufika hatua hii," alisema Al-Hamad.