1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yamtema Mfaransa Migne

13 Agosti 2019

Shirikisho la Soka la Kenya, FKF, linasema limeagana na kocha wake wa timu ya taifa, Sebastien Migne, raia wa Ufaransa ambaye amekuwa akiifunza Harambee Stars, licha ya kufanikiwa pakubwa kwenye ufundishaji wake.

https://p.dw.com/p/3Np3s
Afrika-Cup 2019 | Kenia vs. Senegal
Picha: Reuters/S. Salem

Migne, mwenye umri wa miaka 46, amesifiwa kwa kazi nzuri na ustadi wa kiwango cha juu vilivyopelekea timu hiyo ya taifa ya Kenya kuingia katika kinyang'anyiro cha Kombe la Mataifa ya Afrika (CAF) mwaka huu nchini Misri.

Ilikuwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka 15 kwa Harambee Stars kuingia katika kinyang'anyiro hicho.

FKF inasema utaratibu wa kumteuwa atakayeshika nafasi ya Migne umeshaanza na kuelezea matumaini ya kumtangaza atakayeshika nafasi hiyo hivi karibuni.

Migne aliiongoza Harambee Stars kwa muda wa miezi 15 lakini enzi yake imemalizika kwa kupoteza mechi kupitia mikwaju ya penalti dhidi ya Tanzania kuweza kuwakilishwa katika michuano ya vilabu bingwa barani Afrika mwaka 2020.