Kenya yaelekea wapi? | Matukio ya Afrika | DW | 26.06.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Kenya yaelekea wapi?

Mwishoni mwa miaka ya '60, mshairi Abdilatif Abdulla kutoka pwani ya Kenya aliwahi kuandika shairi akiuliza "Kenya Twendapi?", swali ambalo hadi sasa limesalia bila majibu, hasa kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama.

Mkaazi wa Mpeketoni, Kaunti ya Lamu, Kenya, akibeba bango la kutaka amani baada ya mashambulizi ya hivi karibuni.

Mkaazi wa Mpeketoni, Kaunti ya Lamu, Kenya, akibeba bango la kutaka amani baada ya mashambulizi ya hivi karibuni.

Katika kipindi hiki cha Maoni Mbele ya Meza ya Duara, Mohammed Khelef anaongoza mjadala unaomulika uwezekano wa mdahalo wa kisiasa katika taifa hilo la mashariki ya Afrika, na uwezekano wa mdahalo huo kuokoa hali isielekee kubaya zaidi.

Washiriki wa mjadala huu ni Tom Odhiambo, Koigi Wamwere, Ezekieh Gikambi na Aden Mwachu. Kusikiliza makala nzima, bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman

Sauti na Vidio Kuhusu Mada