Kenya yaangamiza bunduki 5,000 | Matukio ya Afrika | DW | 16.11.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

KENYA

Kenya yaangamiza bunduki 5,000

Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, anasema zaidi ya bunduki 5,200 zimeteketezwa kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki katika jitihada za kuzuia mzunguko wa silaha kuyafikia makundi ya kihalifu.

Ruto aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba serikali imeteketeza bunduki hizo hadharani ili kutuma ujumbe kwa wale wanaofanya biashara haramu ya silaha. 

Makamu huyo wa rais amesema silaha ndogo ndogo zinaleta kitisho kwa amani na utulivu wa Kenya kwa sababu zimekuwa ni rahisi kupatikana kwa bei nafuu na ni nyepesi kuzificha. 

Silaha hizo zilizokamatwa kutoka kwa wahalifu au kusalimishwa kwa hiari ziliharibiwa mjini Ngong, kusini magharibi mwa mji mkuu, Nairobi.

Ruto amewataka wale wote wanaomiliki silaha kinyume na sheria kuzisalimisha kwa jeshi la polisi. 

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com